Tuesday, June 7, 2016
MATUMIZI YA SIMU ZA MKONONI
PATA MAFUNDISHO NA BURUDANI KUTOKA KWA WAIMBAJI WA SHENGENA GOSPEL PANORAMA
Monday, June 6, 2016
EU: UCHAGUZI 2015 ULIHESHIMU KATIBA NA MISING YA KIDEMOCRASIA
Pia kulikuwa na wagombea 1,218 katika nafasi za Ubunge katika majimbo 264, na wagombea 10,879 walijitosa nafasi ya udiwani kwa upande wa Tanzania Bara wakati kwa Zanzibar kulikuwa na wagombea 180 kwa ajili ya majimbo 54 ya Baraza la Uwakilishi, pamoja na wagombea 353 kwa ajili ya halmashauri 111 za mitaa (masheha).
Katika uchaguzi huo, John Magufuli (CCM) alishinda kiti cha urais kwa asilimia 58.46 na kufuatiwa na Edward Lowassa (Chadema) aliyepata asilimia 39.97 huku Anna Mghwira (ACT-Wazalendo) akipata asilimia 0.65.
Kwa upande wa Zanzibar, ushindi ulikwenda kwa Dk Ali Mohamed Shein kwa asilimia 91.4 na kufuatiwa na Hamad Rashid Mohamed aliyepata asilimia tatu. Katika kuhakikisha kunakuwa na uwazi katika mchakato wa uchaguzi huo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC) zilitoa mwaliko kwa taasisi mbalimbali kufanya uangalizi wa uchaguzi huo na moja wa waangalizi hao ni Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya (EU EOM).
EU EOM ilikuwepo nchini kuanzia Septemba 11 hadi Desemba 8 2015, ikituma waangalizi 141 nchini kote kutoka nchi zote 28 wanachama wa EU, pamoja na Norway, Uswisi na Canada. Ujumbe ulitathmini ni kwa kiasi gani mchakato wa uchaguzi ulizingatia ahadi za kitaifa na za kikanda kuhusu uchaguzi, pamoja na sheria za Tanzania. Tathmini ya EU EOM waliyoitoa Juni mwaka huu kuhusu uchaguzi mkuu, zinaonesha kuwa uchaguzi ulionesha dhamira ya Watanzania ya kuzingatia mfumo wa kikatiba na pia kuheshimu misingi ya kidemokrasia.
Chaguzi zote mbili, yaani za Muungano na Zanzibar, zilikuwa na ushindani mkali na kwa kiasi kikubwa ziliendeshwa vyema. Akiwasilisha ripoti ya Umoja wa Ulaya, Mwangalizi Mkuu wa ujumbe huo, Judith Sargentini ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Ulaya anasema, taasisi za usimamizi wa uchaguzi zilionesha viwango vya kutosha vya kujiandaa pamoja na uwezo wa kuendesha hatua muhimu katika kuandaa uchaguzi, kuelekea uchaguzi na pia siku ya uchaguzi.
“Tathmini chanya juu ya kuaminika kwa uendeshaji wa uchaguzi siku ya uchaguzi ilihusu pia Zanzibar.” Sargentini anasema hakuna masharti magumu kujiandikisha kama mpiga kura kwa uchaguzi wa Muungano, ingawa kwa Zanzibar uandikishwaji ulihitaji mtu kuwa na kitambulisho pamoja na ukazi wa miezi 36. Sargentini anasema NEC na ZEC zilionesha kujiandaa vya kutosha kwa utendaji wa mchakato wa uchaguzi na uwezo wa kuendesha operesheni muhimu kama vile uchapishwaji wa karatasi za kupigia kura na kusambaza nyenzo za uchaguzi.
“Pamoja na kutokuwa na muundo wa kudumu kwenye ngazi za chini, EU EOM imeona utendaji wake kuwa wenye mpangilio na ulioandaliwa vizuri. Hata hivyo, katika utekelezaji wa hatua tofauti za mchakato wa uchaguzi, NEC na ZEC hawakuonesha uwazi kamili kuhusu utaratibu wa kufanya maamuzi,” anasema.
Kampeni Sargentini anasema EU EOM ilifanya uangalizi katika matukio 139 ya kampeni na kuwa wagombea na vyama walifanya kampeni kwa ari kubwa, na kwa kiasi kikubwa waliheshimu taratibu za kampeni, ikiwa ni pamoja na kuepuka matumizi ya lugha chochezi na kuzingatia muda uliopangwa kwa ajili ya kampeni.
“Kwa kiasi kikubwa kampeni zilikuwa tulivu na za amani pamoja na hali chanya ya ushindani kwa uchaguzi wa Tanzania Bara, mabishano kati ya mashabiki wa vyama vinavyopingana katika baadhi ya maeneo yaliishia kwa vurugu, matukio hayo yalikuwa kidogo.
“Vyama vya siasa na wagombea walifanya kampeni kwa uhuru katika maeneo yote ya Tanzania Bara wakati kwa upande wa Zanzibar hali ya mvutano ilikuwapo kati ya CCM na CUF, jambo lililosababisha kampeni kali zaidi na gawanyishi, matamshi makali ya baadhi ya viongozi wa vyama yalichangia hali kutokuwa na uvumilivu na kuongeza mvutano miongoni mwa jamii.”
Uwakilishi wa wanawake Sargentini anasema kwa mara ya kwanza CCM ilimteua mwanamke kwa nafasi ya Makamu wa Rais na kulikuwa na mwanamke mmoja aliyeteuliwa na ACT- Wazalendo kuwa miongoni mwa wagombea wanane wa urais wa Muungano. “ Japokuwa katiba zote mbili zinatoa nafasi za viti maalumu kwa ajili ya wanawake ndani ya Bunge na Baraza na wawakilishi, wanawake walikuwa na uwakilishi mdogo katika kugombea viti vya kuchaguliwa na uzungumzaji kwenye mikutano ya kampeni,” anasema.
Upigaji kura Sargentini anasema EU iliona kazi ya kupiga kura ilikuwa chanya, wawakilishi wa vyama walikuwepo kwenye vituo vyote vya kupigia kura, taratibu za upigaji kura zikifuatwa na kuwapo usalama wa kutosha kuhakiki uhalali wa kura na uwazi wa mchakato. “Kazi ya kuhesabu kura ilianza mara baada ya kufunga vituo na liliendeshwa mbele ya mawakala wa vyama vya siasa ambapo walipokea nakala ya fomu ya matokeo.
EU iliona kazi ya ujumlishaji ilikuwa nzuri kwa ujumla na mawakala waliweza kuhakiki takwimu kabla ya kuanza kufanyiwa kazi kwa njia ya elektroniki.” Anasema, tathmini chanya juu ya kuaminika kwa uendeshaji wa uchaguzi siku ya uchaguzi ilihusu pia Zanzibar. “Kufuatia uamuzi wa ZEC kufuta matokeo ya uchaguzi Zanzibar, EU EOM pamoja na waangalizi wengine wa kimataifa, katika tamko la pamoja, walielezea wasiwasi wao mkubwa na kuiomba ZEC iwasilishe ushahidi wa kuhalalisha uamuzi huo...Ushahidi huo haujawahi kuwasilishwa.
EU EOM haikufanya uangalizi wa uchaguzi wa marudio (wa Machi 20, 2016) kwa kuona kuwa mazingira hayakupelekea uchaguzi shirikishi, halisi na wa kuaminika.” Mapungufu Sargentini anasema pamoja na mambo chanya yaliyokuwapo kwenye uchaguzi, lakini kuna mapungufu kadhaa yanayopaswa kuangaliwa kuhusu mfumo wa kiuchaguzi pamoja na utendaji wa mchakato wa uchaguzi kupitia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).
“Zaidi ya hayo, taasisi za usimamizi wa uchaguzi hazikuonesha uwazi kamili juu ya michakato yao ya kufanya maamuzi,” anasema. Mapendekezo Sargentini anasema mapendekezo yao ni pamoja na uwepo wa wagombea binafsi, kuruhusu haki ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais na haki ya vyama vya siasa kuunda umoja wa kiuchaguzi (kama ilivyo Kenya).
Anasema pia, kuendelezwa kwa muundo wa kudumu wa NEC katika ngazi za mikoa, na marekebisho ya mchakato wa uteuzi wa makamishna wa uchaguzi wa NEC na ZEC na kuangaliwa upya mchakato wa uandikishwaji wa wapiga kura Zanzibar ili kuhakikisha ushirikishi zaidi pamoja na imani ya wapiga kura. EU inashauri serikali kuangaliwa upya mipaka ya majimbo ili kuhakikisha usawa zaidi wa kura, muundo huru na wa kudumu wa NEC katika ngazi za mikoa na mabadiliko katika taratibu za uteuzi wa makamishna wa NEC na ZEC ili kuongeza imani juu ya uhuru wao.
Inataka pia maamuzi ya NEC na ZEC yaweze kupingwa mahakamani kipindi kizima cha mchakato kwa maana ya kwamba wanaolalamika wasilazimishwe kusubiri hadi matokeo kutangazwa ili kutafuta njia ya kupata haki.
“Ninafurahi sana kuwasilisha ripoti kamili ambayo inajumuisha yote tuliyoyaona wakati wa uangalizi wetu katika kipindi cha miezi mitatu ambapo ujumbe umekuwepo nchini, pamoja na mapendekezo ya kina kwa chaguzi zijazo.
“Umoja wa Ulaya unaendelea kusimamia dhamira yake ya kufanya kazi na washirika wake Tanzania kuimarisha mchaka- to wa kide- mokrasia nchini, na utaendelea kutazama kwa karibu marekebi- sho ya kiuchaguzi nchini katika miezi na miaka ijayo,” anasema Sargentini.
UKIJUA JEMA LIKAMILISHE
Pata mafundisho bora na burudani ya shengena gospol panorama
Saturday, June 4, 2016
NANI MGANGA MGANGA WA KWELI NI YESU
BURUDIKA NA SHENGENA GOSPOL PANORAMA KWAYA KUTOKA CHOME WILAYANI SAME
Friday, June 3, 2016
MAFUNDISHO NA MAONI
UNGANA NA SHENGENA KWAYA KUTOKA CHOME WILWYANI SAME
MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO NI KUTOKA KWA MR ELIHURUMA CHAO NA YOTE HAYA NI NDANI YA NICE MEDIA PRODUCTION
Thursday, June 2, 2016
BUNGE LA HADHARANI LA SERICAL YA WANAFUNZI KATIKA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA
Kikao cha bunge la wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari kilichowakutanisha baadhi mawaziri
kutoka wizara tofauti tofauti kwa lengo la kuwasilisha ripoti na kujibu maswali ya wabunge hao.
Wizara ambazo zilitakiwa kuwasilisha ripoti zao ni wizara ya Habari,fedha,wizara ya sheria na maadili pamoja na wizara ya afya ulinzi na makazi.Kutokana na wingi wa maswali mengi kwa wizara ya habari hivyo kupelekea wizara nyingine kutowasilisha ripoti
Tuesday, May 31, 2016
NGUVU KAZI NI TEGEMEZI HAPA NCHINI TANZANIA
Vijana nchini washauriwa kujiunga na mashirika ya kujitolea ili wajiongezee ujuzi na maarifa
Vijana nchini Tanzania wameshauriwa kuwa tayari kufanya kazi kwa kujitolea ili kujiongezea ujuzi, uwezo, maarifa na kuleta mabadiliko katika jamii zao,hayo yalielezwa na Meneja wa Maendeleo ya Vijana wa shirika la Raleigh Tanzania, Genos Martin wakati wa mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii.
Martin alisema kuwa ni vyema kwa vijana kujiunga na mashirika ya kitaifa na ya kimataifa ya kujitolea kwani kwa kufanya hivyo kutawapa vijana fursa ya kuongeza ujuzi na maarifa ambao utawasaidia katika sehemu mbalimbali.
Martin alisema, "Kufanya kazi kwa kujitolea ni kitu kigeni nchini kwetu tofauti na Mataifa ya nchi zilizoendelea, watu waliowahi jitolea wanapewa kipaumbele kwenye maombi ya kazi tofauti na nchini kwetu. Hii inafanya kujitolea kuwa jambo la muhimu sana kwenye mataifa ya wenzetu"
"Vijana wengi wanalalamika kuwa nafasi nyingi za kazi zinawataka wawe na uzoefu wa miaka mitatu nakuendelea, hawajui ni vipi wanaweza kupata uzoefu lakini kama wakijiunga na haya mashirika ya kujitolea wanaweza pata huo uzoefu na kuwafanya wawe na nafasi nzuri pindi waombapo ajira" aliongezea Martin.
Aidha, Afisa Mawasiliano wa Raleigh Tanzania, Kennedy Mmari alieleza kuwa ni kawaida ya shirika hilo kutafuta vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini ambao huungana na vijana wenzao kutoka mataifa ya mbali mbali ya Ulaya na Amerika.
Mmari aliongezea, "Raleigh tuna programu kwa vijana zinazohusu ujasiriamali, usafi, maji na utunzaji wa mazingira, kijana yeyote anaweza kujjiunga nasi na kufanya program zetu. Hatutoi malipo yoyote wala hawatulipi chochote isipokuwa tunagharamia mahitaji yao yote ya msingi pindi wakiwa kwenye programu"
Wanafunzi wa shule ya Msingi Chibe iliyopo kata ya Old Shinyanga mkoani Shinyanga wakishuhudia ufunguzi wa kituo cha elimu ya awali kilichojengwa na na vijana wa kujitolea kwa msaada wa shirika la Raleigh Tanzania.
Kwa upande wa vijana waliofanya programu na shirika hilo wameshukuru kwa nafasi waliyopewa kwani imewasaidia kupata ujuzi na ufahamu wa mambo tofauti ikiwemo jinsi ya kuandaa na kusiammia biashara.
Mmoja wa vijana ambao wamepata fursa hiyo, Sia Malamsha, alisema kuwa anajiona wa tofauti baada ya kumaliza programu, hakuwahi fikiria kama kuna watu Tanznaia hawana huduma za maji safi na salama lakini kupitia programu za Raleigh nimeweza fika kwenye jamii hizo na kuwasaidia kutatua matatizo hayo.
"Nimekuwa sehemu ya mabadiliko makubwa katika nchi yangu, najivunia kuona nimefanya kitu kuikomboa jamii ya Watanzania" aliongezea Bi. Malamsha.
Vijana wa Shirika la kujitolea la Raleigh wakishiriki ujenzi wa choo katika moja ya miradi yao
|
Naye kijana Ashiru Said aliyefanya programu ya ujasiriamali amesema kua programu za Raleigh zimemsaidia kupata elimu ya kusimamia na kuendesha biashara.
"Nimeweza kupata elimu ya ujasiriamali, baada ya kurudi nyumbani jamii imefaidika na elimu niliyoipata kwani nimeweza waelimisha vijana wenzangu jinsi ya kuanzisha na kusimamia biashara zao wenyewe" alimalizia Said.
Raleigh Tanzania ni shirika lisilo la kiserikali lenye ofisi zake mkoani Morogoro na kufanya programu za kujitolea kwa lengo la kuisaidia jamii ya Tanzania sehemu mbalimbali.
Monday, May 30, 2016
YALIYOJIRI NDANI YA BUNGE LA MUUNGANO WA TANZANIA
Wabunge wakiondoka ndani ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya Naibu Spika kutangaza kuahirisha shughuli za Bunge leo.
Wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiwa wamesimama ndani ya ukumbi wa Bunge kufuatia Naibu Spika wa Bunge hilo Mhe. Tulia Ackson kutangaza kuliahirisha Bunge leo mjini Dodoma.Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson Mwansasu akiongoza kikao cha 32 cha Mkutano wa tatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.
Baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri wakifuatilia masuala mbalimbali ndani ya Ukumbi wa Bunge wakati wa kikao cha 32 cha Bunge hilo mjini Dodoma
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla akijibu maswali ya wabunge kuhusu sekta ya Afya Bungeni mjini Dodoma.
Mbunge wa jimbo la Ukonga (CHADEMA) Mhe. Mwita Mwikwabwe akisoma kitabu cha Kanuni za Kudumu za Bunge ndani ya Ukumbi wa Bunge.
Mbunge wa Nzega Mhe. Hussein Bashe (CCM) akizungumza jambo na Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) Mhe. Joshua Nassari (kulia) nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kuahirishwa kwa kikao cha 32 cha mkutano wa tatu wa Bunge leo mjini Dodoma.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Barbro Johansson iliyoko jijini Dar es salaam wakiondoka ndani ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Sulemani Jafo akijibu maswali ya wabunge yaliyoelekezwa kwenye wizara yake Bungeni mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Suzan Kolimba nje ukumbi wa Bunge.
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Thomas Kashililah (kulia) akizungumza jambo na wabunge leo mjini Dodoma.
Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) Mhe. Joshua Nassari (kushoto) akisisitiza jambo kwa Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Andrew Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Mbunge wa Kigoma Mhe. Peter Selukamba akijadiliana jambo na Mbunge wa Nzega mjini Mhe. Hussein Bashe (kushoto)Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu nje ya Ukumbi wa Bunge mjini.
Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) Mhe. Joshua Nassari (kushoto) akimweleza jamboMwenyekiti wa Bunge Mhe. Andrew Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma. PICHA/Aron Msigwa na Fatma Salum - DODOMA
Friday, May 27, 2016
USHINDI WA KISHINDO NDANI YA AJTC CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI WAPATIKANA . JE NANI BINGWA KATIKA UTANGAZAJI?
Darasa la Mbuga ya Ngorongoro katika chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha(Ajtc) wakishangilia mara baada ya kuibuka washindi katika michuano ya utangazaji iliyofanyika chuoni hapo. |
Michuano ya utangazaji katika chuo cha uandishi wa habari na utangaza Arusha
(A.J.T.C) imemalizika hii leo ambapo mshindi wa kwanza hadi wa mwisho amejulikana.
Darasa lililoibuka kidedea katika mashindano hayo yaliyochukua takribani siku tano linatambulika kwa jina la Mbuga ya Ngorongorongoro.
Mashindano hayo yaliyohusisha madasa 13, darasa la Ngorongoro limejishindia kombe lenye thamani ya Tsh 10,000 pamoja na pesa taslimu Tsh 150,000.
Nafasi ya pili katika michuano hiyo Utangazaji ilichukuliwa na darasa linaloitwa Mlima Kilimanjaro huku wakijinyakulia Tsh10,000.
Darasa la Serengeti limeshikilia nafsi ya tatu na kupewa zawadi fedha taslimu Tsh 75,000.
Mkurugenzi wa chuo hicho cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha bw Joseph Mayagila amewapongeza wanafunzi wote walioshiriki na kuwataka waendelee kujituma katika masomo yao ili wafanye vizuri katika tasnia ya uandishi wa habari na utangazaji.
Monday, May 23, 2016
JE NANI BINGWA WA KUTANGAZA NDANI YA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA
Mashindano ya Utangazaji katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha katika mwaka 2016 yameanza rasmi siku ya leo.Mashindano hayo ni ya 9 tangu kuanzishwa kwa chuo hichi cha utangazaji.Takribani madarasa 13 yatashiriki na leo yameanza madarasa 3.Madarasa hayo ni pamoja na darasa la Selous,Mt. Evarest na darasa la Mt. Meru na mashindano haya ni maalumu kwa wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho na lengo kuu la mashindano hayo ni kujifunza na kuwanoa wanafunzi hao ili wanapomaliza chuo wawe na uzoefu wa utangazaji
Mashindano hayo yanatarajia kufikia tamati siku ya Ijumaa ambapo mshindi wa kwanza atajinyakulia Kombe lenye thamani ya sh. 100,000/= na pesa taslimu sh. 150,000/= ,Mshindi wa pili atapata zawadi ya pesa sh. 100,000/= na mshindi wa tatu atapata pesa Sh. 75,000/=
Kesho mashindano yataendelea kwa madarasa yafuatayo;
Darasa la Mt. Udzungwa, kisha darasa la Serengeti na kumaliziwa na darasa la Aicc
Makamo mkuu wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bw. Elifuraha Samboto akifungua rasmi mashindano ya utangazaji katika chuo hicho ambaye pia ni mshauri mkuu wa kamati ya utangazaji chuoni hapo.
Bw. Elifuraha Samboto akitoa maneno mafupi kabla ya ufunguzi wa mashindano ya utangazaji
Mkuu wa kitengo cha utangazaji katika chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bw. Onesmo Mbise akitoa maelekezo kwa wanafunzi jinsi ya kutumia vifaa vya utangazaji kabla ya mashindano kuanza
Mwanafunzi kutoka darasa la Mt meru Teobad jacobo akijaribu vifaa kabla matangazo hayajaanza
Friday, May 20, 2016
UFUNGUZI WA MASHINDANO YA UTANGAZAJI YAMEFUNGULIWA RASMI NA WALIMU WA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA{ AJTC}
Kama ilivyo ada mwalimu lazima amuonyeshe mwanafunzi kwamba nini kinatakiwa kufanyika?
Mkufunzi wa AJTC Bw Andrea Ngobole ndani ya studio za 96.6 AJTC FM |
ELIHURUMA CHAO Mkufunzi wa Maswala ya Production na Fundi Mitambo wa AJTC Radio akiwa Katika studio za Radio kuhakikisha Mitambo Inakaa sawa |
Makamu Mkuu wa chuo cha Uandishi Wa habari na Utangazaji Arusha Bw. ELIFURAHA SAMBOTO Akiwasilisha Taarifa ya Habari |
JACKLINE JOELI Mkufunzi wa Arusha Journalism Akiwa katika kipindi cha GOSPEL TIME Cha 96.6 AJTC RADIO |
ONESMO ELIA MBISE kulia Mkufunzi wa Chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha pia ni Mkuu wakitengo Cha utangazaji Chuoni hapo akiwa katika kipindi cha ELIMIKA NAMI |
Pichani Ni STEPHEN MULAKI Katika Makala Murua ya DUNIA Makala inayohusiana na Watu wenye Ulemavu wa ngozi ALBINO |
Monday, April 25, 2016
MAKAMU WA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA BW ELIFURAHA SAMBOTO AKITOA SEMINA YA UJASIRIAMALI NAMNA YA KUTAFUTA MASOKO |
mitazamo ya ukosefu wa ajira kwa vijana wengi itakoma, kwa jitiada za wakufunzi wa chuo hicho kuakikisha kuwa mwanafunzi anatoka hapo akiwa na mtazamo wakujiajiri na kuanzisha kilicho chake.
Vijana wengi wamekuwa wakilalamikia tatizo la ajira huku wakitupia serikali lawama za hapa na pale wakisaau kuwa uchumi unajengwa na mtu binafsi kwa nguvu zake na jitiada zake.
UMASKINI ni nini basi
ni hile hali ya ukosefu wa mahitaji ya msingi kwa binadamu kama vile chakula, maji safi, huduma za afya, mavazi na malazi kutokana na kukosa uwezo wa kuvinunua.
Kutokuwa na rasilimali za kutosha husababisha pato la taifa kupungua hali inayoifanya serikali kukosa fedha za kuboreshea huduma za jamii.
Afya duni na ukosefu wa elimu pia ni vishairia vya umaskini kwani wananchi wasipokuwa na afya na elimu hawawezi kuzalisha bidhaa bora zinazoweza kushindanishwa katika soko la dunia.
Ujasiriamali ni nini basi?
Ujasiriamali ni ile hali ya kuwa radhi kuthubutu au kuanzisha jambo jipya kwa njia ya ubunifu ambao utampa faida hapo baadaye baada ya kunadi ufanisi wake kwani hata wanauchumi wengi wanakubali kuwa ujasiriamali ni kiungo muhimu katika kukuza na kuendeleza uchumi wa Taifa.
Wengi wao hutazama ujasiriamali kama vile upo kwa ajili ya watu ambao hawana kazi. Siwalaumu wote wenye mtazamo wa aina hiyo kwani haya ni matokeo ya mfumo wa uchumi uliotukuza pia ni mfumo unaoamini kuwa mafanikio ya kweli yanapatikana kwa mtu kusoma na kisha kuajiriwa.
Licha ya hayo, kwa kipindi kirefu sasa serikali na sekta binafsi zimeshindwa kukidhi wimbi la vijana wanaomaliza shule ama vyuo hivyo basi wakati umefika wa kushawishi vijana kuangalia na kutafuta mbinu mpya za kujiajiri kama wajasiriamali ili kuweza kujikimu katika maisha yao ya kila siku.
Ikumbukwe kuwa utajiri utokanao na ujasiriamali ama kufanya kazi kwa bidii au umaskini wa mtu huanzia katika fikra na mitazamo yake kwani tajiri huwa tajiri kabla hajamiliki mali yoyote na maskini huwa maskini kabla ya kuridhika na hali yake.
Ujasiriamali ni zaidi ya kuanzisha biashara na hata wale waliojiriwa wanaweza kuwa wajasiriamali kwenye kazi zao kwa kuwa wabunifu na kuanzisha mbinu mpya zitakazorahisisha kazi zao na kuleta ufanisi ili kuepuka kuwa wabangaizaji na wahangaikaji ilihali tukitaka kuitwa wajasirimali.
KUNAFAIDA NYINGI SANA KUWA MJASIRIAMALI
1. Inatusaidia kutatua maitaji ya watu na jamii kwa ujumla kwani nikuleta majibu ya matatizo ya wengi
2.Faida nyingine za ujasiriamali ni kwamba hutusaidia kutumia ipasavyo rasilimali tulizo nazo, kupelekea kwenye matumizi sahihi ya rasilimali watu pia hutupa mwanga katika kufanya na kuanzisha shughuli mpya pamoja na kupunguza idadi ya watu tegemezi baada ya kujipatia kipato.
3.Hali kadhalika ujasiriamali ni njia mbadala ya kuongeza nafasi za ajira katika nchi zinazoendelea kwani ni msingi katika kujiongezea kipato na kupunguza umaskini, hivyo basi ni wajibu wa serikali kusaidia wajasiriamali wakubwa na wadogo ili kuongeza tija katika uzalishaji wa bidhaa na huduma kutoa mchango chanya katika mipango ya maendeleo ya nchi au taifa husika.
Shukrani kwa wakufunzi wote wa ARUSHA JOURNALISM TRAINING COLLEGE
Subscribe to:
Posts (Atom)