Tuesday, June 7, 2016
MATUMIZI YA SIMU ZA MKONONI
PATA MAFUNDISHO NA BURUDANI KUTOKA KWA WAIMBAJI WA SHENGENA GOSPEL PANORAMA
Monday, June 6, 2016
EU: UCHAGUZI 2015 ULIHESHIMU KATIBA NA MISING YA KIDEMOCRASIA
Pia kulikuwa na wagombea 1,218 katika nafasi za Ubunge katika majimbo 264, na wagombea 10,879 walijitosa nafasi ya udiwani kwa upande wa Tanzania Bara wakati kwa Zanzibar kulikuwa na wagombea 180 kwa ajili ya majimbo 54 ya Baraza la Uwakilishi, pamoja na wagombea 353 kwa ajili ya halmashauri 111 za mitaa (masheha).
Katika uchaguzi huo, John Magufuli (CCM) alishinda kiti cha urais kwa asilimia 58.46 na kufuatiwa na Edward Lowassa (Chadema) aliyepata asilimia 39.97 huku Anna Mghwira (ACT-Wazalendo) akipata asilimia 0.65.
Kwa upande wa Zanzibar, ushindi ulikwenda kwa Dk Ali Mohamed Shein kwa asilimia 91.4 na kufuatiwa na Hamad Rashid Mohamed aliyepata asilimia tatu. Katika kuhakikisha kunakuwa na uwazi katika mchakato wa uchaguzi huo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC) zilitoa mwaliko kwa taasisi mbalimbali kufanya uangalizi wa uchaguzi huo na moja wa waangalizi hao ni Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya (EU EOM).
EU EOM ilikuwepo nchini kuanzia Septemba 11 hadi Desemba 8 2015, ikituma waangalizi 141 nchini kote kutoka nchi zote 28 wanachama wa EU, pamoja na Norway, Uswisi na Canada. Ujumbe ulitathmini ni kwa kiasi gani mchakato wa uchaguzi ulizingatia ahadi za kitaifa na za kikanda kuhusu uchaguzi, pamoja na sheria za Tanzania. Tathmini ya EU EOM waliyoitoa Juni mwaka huu kuhusu uchaguzi mkuu, zinaonesha kuwa uchaguzi ulionesha dhamira ya Watanzania ya kuzingatia mfumo wa kikatiba na pia kuheshimu misingi ya kidemokrasia.
Chaguzi zote mbili, yaani za Muungano na Zanzibar, zilikuwa na ushindani mkali na kwa kiasi kikubwa ziliendeshwa vyema. Akiwasilisha ripoti ya Umoja wa Ulaya, Mwangalizi Mkuu wa ujumbe huo, Judith Sargentini ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Ulaya anasema, taasisi za usimamizi wa uchaguzi zilionesha viwango vya kutosha vya kujiandaa pamoja na uwezo wa kuendesha hatua muhimu katika kuandaa uchaguzi, kuelekea uchaguzi na pia siku ya uchaguzi.
“Tathmini chanya juu ya kuaminika kwa uendeshaji wa uchaguzi siku ya uchaguzi ilihusu pia Zanzibar.” Sargentini anasema hakuna masharti magumu kujiandikisha kama mpiga kura kwa uchaguzi wa Muungano, ingawa kwa Zanzibar uandikishwaji ulihitaji mtu kuwa na kitambulisho pamoja na ukazi wa miezi 36. Sargentini anasema NEC na ZEC zilionesha kujiandaa vya kutosha kwa utendaji wa mchakato wa uchaguzi na uwezo wa kuendesha operesheni muhimu kama vile uchapishwaji wa karatasi za kupigia kura na kusambaza nyenzo za uchaguzi.
“Pamoja na kutokuwa na muundo wa kudumu kwenye ngazi za chini, EU EOM imeona utendaji wake kuwa wenye mpangilio na ulioandaliwa vizuri. Hata hivyo, katika utekelezaji wa hatua tofauti za mchakato wa uchaguzi, NEC na ZEC hawakuonesha uwazi kamili kuhusu utaratibu wa kufanya maamuzi,” anasema.
Kampeni Sargentini anasema EU EOM ilifanya uangalizi katika matukio 139 ya kampeni na kuwa wagombea na vyama walifanya kampeni kwa ari kubwa, na kwa kiasi kikubwa waliheshimu taratibu za kampeni, ikiwa ni pamoja na kuepuka matumizi ya lugha chochezi na kuzingatia muda uliopangwa kwa ajili ya kampeni.
“Kwa kiasi kikubwa kampeni zilikuwa tulivu na za amani pamoja na hali chanya ya ushindani kwa uchaguzi wa Tanzania Bara, mabishano kati ya mashabiki wa vyama vinavyopingana katika baadhi ya maeneo yaliishia kwa vurugu, matukio hayo yalikuwa kidogo.
“Vyama vya siasa na wagombea walifanya kampeni kwa uhuru katika maeneo yote ya Tanzania Bara wakati kwa upande wa Zanzibar hali ya mvutano ilikuwapo kati ya CCM na CUF, jambo lililosababisha kampeni kali zaidi na gawanyishi, matamshi makali ya baadhi ya viongozi wa vyama yalichangia hali kutokuwa na uvumilivu na kuongeza mvutano miongoni mwa jamii.”
Uwakilishi wa wanawake Sargentini anasema kwa mara ya kwanza CCM ilimteua mwanamke kwa nafasi ya Makamu wa Rais na kulikuwa na mwanamke mmoja aliyeteuliwa na ACT- Wazalendo kuwa miongoni mwa wagombea wanane wa urais wa Muungano. “ Japokuwa katiba zote mbili zinatoa nafasi za viti maalumu kwa ajili ya wanawake ndani ya Bunge na Baraza na wawakilishi, wanawake walikuwa na uwakilishi mdogo katika kugombea viti vya kuchaguliwa na uzungumzaji kwenye mikutano ya kampeni,” anasema.
Upigaji kura Sargentini anasema EU iliona kazi ya kupiga kura ilikuwa chanya, wawakilishi wa vyama walikuwepo kwenye vituo vyote vya kupigia kura, taratibu za upigaji kura zikifuatwa na kuwapo usalama wa kutosha kuhakiki uhalali wa kura na uwazi wa mchakato. “Kazi ya kuhesabu kura ilianza mara baada ya kufunga vituo na liliendeshwa mbele ya mawakala wa vyama vya siasa ambapo walipokea nakala ya fomu ya matokeo.
EU iliona kazi ya ujumlishaji ilikuwa nzuri kwa ujumla na mawakala waliweza kuhakiki takwimu kabla ya kuanza kufanyiwa kazi kwa njia ya elektroniki.” Anasema, tathmini chanya juu ya kuaminika kwa uendeshaji wa uchaguzi siku ya uchaguzi ilihusu pia Zanzibar. “Kufuatia uamuzi wa ZEC kufuta matokeo ya uchaguzi Zanzibar, EU EOM pamoja na waangalizi wengine wa kimataifa, katika tamko la pamoja, walielezea wasiwasi wao mkubwa na kuiomba ZEC iwasilishe ushahidi wa kuhalalisha uamuzi huo...Ushahidi huo haujawahi kuwasilishwa.
EU EOM haikufanya uangalizi wa uchaguzi wa marudio (wa Machi 20, 2016) kwa kuona kuwa mazingira hayakupelekea uchaguzi shirikishi, halisi na wa kuaminika.” Mapungufu Sargentini anasema pamoja na mambo chanya yaliyokuwapo kwenye uchaguzi, lakini kuna mapungufu kadhaa yanayopaswa kuangaliwa kuhusu mfumo wa kiuchaguzi pamoja na utendaji wa mchakato wa uchaguzi kupitia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).
“Zaidi ya hayo, taasisi za usimamizi wa uchaguzi hazikuonesha uwazi kamili juu ya michakato yao ya kufanya maamuzi,” anasema. Mapendekezo Sargentini anasema mapendekezo yao ni pamoja na uwepo wa wagombea binafsi, kuruhusu haki ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais na haki ya vyama vya siasa kuunda umoja wa kiuchaguzi (kama ilivyo Kenya).
Anasema pia, kuendelezwa kwa muundo wa kudumu wa NEC katika ngazi za mikoa, na marekebisho ya mchakato wa uteuzi wa makamishna wa uchaguzi wa NEC na ZEC na kuangaliwa upya mchakato wa uandikishwaji wa wapiga kura Zanzibar ili kuhakikisha ushirikishi zaidi pamoja na imani ya wapiga kura. EU inashauri serikali kuangaliwa upya mipaka ya majimbo ili kuhakikisha usawa zaidi wa kura, muundo huru na wa kudumu wa NEC katika ngazi za mikoa na mabadiliko katika taratibu za uteuzi wa makamishna wa NEC na ZEC ili kuongeza imani juu ya uhuru wao.
Inataka pia maamuzi ya NEC na ZEC yaweze kupingwa mahakamani kipindi kizima cha mchakato kwa maana ya kwamba wanaolalamika wasilazimishwe kusubiri hadi matokeo kutangazwa ili kutafuta njia ya kupata haki.
“Ninafurahi sana kuwasilisha ripoti kamili ambayo inajumuisha yote tuliyoyaona wakati wa uangalizi wetu katika kipindi cha miezi mitatu ambapo ujumbe umekuwepo nchini, pamoja na mapendekezo ya kina kwa chaguzi zijazo.
“Umoja wa Ulaya unaendelea kusimamia dhamira yake ya kufanya kazi na washirika wake Tanzania kuimarisha mchaka- to wa kide- mokrasia nchini, na utaendelea kutazama kwa karibu marekebi- sho ya kiuchaguzi nchini katika miezi na miaka ijayo,” anasema Sargentini.
UKIJUA JEMA LIKAMILISHE
Pata mafundisho bora na burudani ya shengena gospol panorama
Saturday, June 4, 2016
NANI MGANGA MGANGA WA KWELI NI YESU
BURUDIKA NA SHENGENA GOSPOL PANORAMA KWAYA KUTOKA CHOME WILAYANI SAME
Friday, June 3, 2016
MAFUNDISHO NA MAONI
UNGANA NA SHENGENA KWAYA KUTOKA CHOME WILWYANI SAME
MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO NI KUTOKA KWA MR ELIHURUMA CHAO NA YOTE HAYA NI NDANI YA NICE MEDIA PRODUCTION
Thursday, June 2, 2016
BUNGE LA HADHARANI LA SERICAL YA WANAFUNZI KATIKA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA
Kikao cha bunge la wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari kilichowakutanisha baadhi mawaziri
kutoka wizara tofauti tofauti kwa lengo la kuwasilisha ripoti na kujibu maswali ya wabunge hao.
Wizara ambazo zilitakiwa kuwasilisha ripoti zao ni wizara ya Habari,fedha,wizara ya sheria na maadili pamoja na wizara ya afya ulinzi na makazi.Kutokana na wingi wa maswali mengi kwa wizara ya habari hivyo kupelekea wizara nyingine kutowasilisha ripoti
Subscribe to:
Posts (Atom)