Tuesday, February 16, 2016

Vigogo wanne MSD wasimamishwa kazi





Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwa amebeba vifaa vilivyopelekwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD) Muhimbili jana. (Na Mpigapicha Wetu).
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amemwagiza Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD), kuwasimamisha kazi mara moja wakurugenzi wanne wa taasisi hiyo kutokana na tuhuma za kuwepo matumizi mabaya ya Sh bilioni 1.5.
Wakurugenzi hao ni Mkurugenzi wa Kanda wa MSD, Cosmas Mwaifwani, Mkurugenzi wa Fedha, Joseph Tesha, Mkurugenzi wa Ugavi, Misanga Muja na Mkurugenzi wa Manunuzi, Heri Mchunga.
“Naomba uwaandikie barua za kuwasimamisha wakurugenzi hawa wanne ili wapishe uchunguzi wa matumizi mabaya ya Sh bilioni 1.5 za MSD,” alisema Ummy alipozungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam.
Ummy alisema taarifa alizonazo ni kwamba kiasi hicho cha fedha, kilitumika kununulia dawa kinyume cha utaratibu na Sheria ya Manunuzi ya Umma, hivyo kuna haja ya kufanyika kwa uchunguzi huo.
Uamuzi wa Waziri huyo wa Afya ni mwendelezo wa hatua kadhaa zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano dhidi ya watumishi wa umma ambao wamekuwa wakituhumiwa kujihusisha na vitendo vya ubadhirifu kwa kuchukuliwa hatua katika kile ambacho Rais John Magufuli amekipachika jina la ‘kutumbua majipu.’
Utekelezaji agizo la Magufuli Katika hatua nyingine, Rais Magufuli ya kuwapatia vitanda wanaokwenda kujifungulia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, jana ilitekelezwa baada ya MSD kupeleka vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Sh milioni 89.
Vifaa ambavyo alivikabidhi jana Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu ni vitanda 120, magondoro 120, vitanda 10 vya kujifungulia, mashuka 840 na vitanda kwa ajili ya watoto njiti 10.
“Tumeleta vifaa hivi hapa baada ya kuagizwa na Rais kuwa tulete vifaa hivi kwa ajili ya wodi ya wanawake na Rais ametuhakikishia kuwa fedha hiyo italipwa mara moja,” alisema Bwanakunu wakati akikabidhi vifaa hivyo ambavyo vilipokewa na Waziri Ummy.
Rais alitoa ahadi ya kuwapelekea vitanda wanawake hao baada ya kupita katika wodi hiyo, wakati anatoka kumjulia hali Mufti wa Tanzania, Shehe Abubakary Zubeiry.
Akihutubia Taifa kupitia Wazee wa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Rais Magufuli aliahidi kuwa ahadi yake ya kuwapelekea vitanda wajawazito hao ataitekeleza haraka.
Akipokea vifaa hivyo, Waziri Ummy alimshukuru Rais kwa kuguswa na afya ya wanawake baada ya kupita katika wodi ya wazazi na kukuta baadhi yao wakilala chini.
Alisema akiwa waziri aliyepewa dhamana ya kuongoza wizara hiyo, amefurahishwa kuona Rais hataki masuala ya urasimu ya mchakato, bali anataka kuona mambo yanatekelezwa kwa vitendo.
“Baada ya kupokea vifaa hivi, nakuagiza Mkurugenzi wa Muhimbili, kwamba vitanda hivi vifungwe leo, na akina mama ambao wamebanana kule wodi ya wazazi wahamishiwe katika jengo lingine ambalo litakuwa na vitanda hivi,” alisema Ummy.
Alisema kwa vitendo alivyoonesha Rais Magufuli, atahakikisha kuwa huduma za afya zinatolewa kwa kiwango ambacho wananchi wanapenda kitolewe.
“Rais ameguswa na matatizo ya wananchi wake, sisi ambao tunamsaidia lazima tuwajibike na amenipa msukumo wa ajabu kushughulikia changamoto zinazozikabili hospitali zetu,” alisema.
Hospitali za mikoa na wilaya kukaguliwa Waziri Ummy alimwagiza Katibu Mkuu wa Wizara yake, Dk Mpoki Ulisubisya kumwagiza Mkurugenzi wa Tiba wa wizara hiyo, ahakikishe anakwenda mikoani kukagua matatizo ya hospitali za mikoa na wilaya na kutoa suluhisho la changamoto hizo.
“Badala ya kwenda nje ya nchi, katibu mkuu mwagize mkurugenzi aende wilayani na mikoani huko akajionee hali halisi za hospitali zetu ili tuweze kushughulikia changamoto hizo,” alisema Ummy.
Pia alimwagiza katibu mkuu kwa kushirikiana na mkurugenzi huyo wa Tiba kutoa taarifa kila siku za hali za hospitali za mikoa na wilaya kama kuna wagonjwa ambao wanalala chini ili watatuliwe matatizo.
Aliwataka wakuu wa mikoa na wilaya kutoa taarifa wizarani kila siku kama katika maeneo yao kuna mgonjwa anayelala chini katika hospitali za wilaya na mikoa. “Sitegemei tena mgonjwa alale chini,” alisema.

Wednesday, February 10, 2016

WANAFUNZI 21 WA SHULE YA MSINGI KILAMBO CHAMKOLECHI WAFUKUZWA SHULE KWA KOSA LA KUVAA VIATU AINA YEBOYEBO


Wanafunzi wapatao 21 wanaosoma Shule ya Msingi Kilambo cha Mkolechi, Kata ya Kala mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Nkasi, wamefukuzwa shule kwa muda usiojulikana kwa kuvaa viatu maarufu yeboyebo.

Imeelezwa kwamba yeboyebo hizo zilikusanywa na kuchomwa kwa kile kilichoelezwa kwamba ni kunatokana na waraka uliotolewa na Ofisa Elimu Halmashauri ya Nkasi (Msingi) ukipiga marufuku wanafunzi kuvaa aina hiyo ya viatu shuleni.

Hata hivyo,jana  Ofisa Elimu Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi (Msingi), Misana Kwangula, alikanusha kutoa waraka huo kwa shule hiyo.

“Sina taarifa rasmi ila jana jioni (Jumatatu) alinipigia simu mkazi mmoja akinitaarifu kwamba kuna mwalimu wa shule ya msingi Kilambo cha Mkolechi amechoma moto viatu vya wanafunzi kwa madai kuwa ofisa elimu (msingi) ametoa waraka kwamba wanafunzi hawatakiwi kuvaa yeboyebo shuleni…

“Hakuna waraka wala marufuku yoyote iliyotolewa, isitoshe sio sahihi hata kidogo wala sio kitu kizuri kuchoma vifaa walivyonavyo wanafunzi…. Sasa kama amewachomea wanafunzi hao viatu hivyo vya yeboyebo basi awanunulie viatu vya ngozi,” alisema Kwangula.

Mkasa huo wa wanafunzi hao kufukuzwa shule na kuchomewa yeboyebo walizovaa ulitokea juzi wakati wanafunzi hao walipofika shuleni wakiwa wamevaa viatu hivyo.

Inaelezwa kwamba mwalimu wa zamu, Baraka Mwakasege aliwazuia kuingia darasani, badala yake akawaamuru wavue viatu vyao.

Taarifa kutoka shuleni hapo zinaeleza kuwa, baada ya hatua hiyo, mwalimu huyo wa zamu alizikusanya yeboyebo na kuzitia kiberiti kisha akawafukuza wanafunzi hao kwa muda usiojulikana hadi wazazi na walezi watakapowanunulia viatu vya ngozi.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Posian Ally alikanusha kumtuma mwalimu wa zamu kuwafukuza wanafunzi hao shule kwa muda usiojulikana wala kuteketeza kwa moto yeboyebo zao.

 Alisema ataitisha kikao ili kujadili suala hilo na kwamba mwalimu huyo akibainika kutenda kosa hilo ataamriwa kuwanunulia watoto hao viatu vingine

BASATA WAFUNGIA WIMBO WA NAY WAMITEGO WADAI HAUNA MAADILI


BASATA imetoa kauli hiyo kupitia Katibu mkuu mtendaji wa baraza hilo Godfrey Lebejo, alipokuwa akiongea katika kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwamba anaamini hata kwenye media wimbo huo hautapigwa.
“Ni wimbo ambao haufai na ni msanii ambaye I dont know hata unashindwa kumpima ana akli ya namna gani, au kwa nini ameamua kufanya hivyo, lakini watu kama hao kwenye jamii wapo, ni kazi ambayo haifai katika jamii kwa hiyo kwa mujibu wa sheria na kanuni zake, kitu ambacho hakifai kwenye jamii sio mpaka litolewe tamko kwamba wimbo umefungiwa, ni wimbo ambao haufai hata wanajamii wameona haufai, nadhani mtu mwenye akili timamu kiujumla anajua, najua kwenye media hauwezi kupigwa”, alisema Godfrey.

Katibu huyo wa BASATA amesema kinachotakiwa kwa Ney ni kujitambua kama yeye ni kioo cha jamii, na kwa kufanya vitendo kama hivyo si sahihi kwake kwani jamii inamtazama yeye.

“Anachofanya afikirie yeye ni nani na ana nafasi gani kwenye jamii, kwa sababu mtu anayefanya namna hii asidhani kama anamdhalilisha mtu, anajidhalilisha yeye mwenyewe kwa sababu mtu yeyote ambaye anatoa lugha chafu, anafanya vitendo vya aibu, asidhani kama anamdhalilisha mtu, kwa hiyo yeye mwenyewe ni kama hayawani fulani tu”, alisema Godfrey Lebejo

USHINDI WA CHANI UMEMFANYA RAIS KABILA KUTOA ZAWADI YA GARI KWA KILA MCHEZAJI


Rais wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo Laurent Kabila ameamua kuwazawadia magari wachezaji wa timu ya taifa ya Kongo walioshinda Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza Ligi za ndani (CHAN), Rais Kabila ameagawa magari kwa wachezaji 23 na viongozi 7 waliofanikiwa kutwaa Kombe la CHAN kwa mwaka 2016, michuano ambayo imefanyika Rwanda.
IMG-20160209-WA0020
DR Congo ilifanikiwa kuifunga timu ya taifa ya Mali kwa goli 3-0, na kutwaa taji lake la pili la michuano hiyo, baada ya kufanya hivyo kwa zaidi ya miaka minne nyuma, gari hizo walizopewa wachezaji wa timu ya taifa ya Kongo BBC inataja kuwa zinathamani ya KSH milioni 6 za Kenya kwa Tanzania ni Tsh Milioni 130 kwa kila gari. Michuano ya CHANilikuwa inashirikisha timu 16.
IMG-20160209-WA0028
IMG-20160209-WA0020NNNNNN

AJALI YA KONTENA LILILO GONGANA NA GARI DOGO


Habari zilizoenea kwa kiasi kikubwa kwa watumiaji wa barabara ya Mandela  jijini Dar Es Salaam ni kuhusiana na ajali iliyotokea ya kontena kuangukia basi dogo la abiria maarufu kama daladala na gari ndogo. Ajali hiyo kwa taarifa za awali inatajwa kutokea maeneo yaTabatariziki .com inafuatilia kwa kina taarifa kamili ili kukuletea habari za uhakika zaidi ila hizi ni picha za mwanzo kuhusu ajali hiyo
IMG-20160210-WA0007
IMG-20160210-WA0009

TANZANIA YAFICHUA WIZI WA MILIONI 700



Image copyrightAFP
Image captionRais Magufuli
Serikali ya Tanzania imebaini wizi wa takribani shilingi milioni 700 sawa na dola laki tatu za marekani ($320,000 )katika shirika lake la Ndege (ATCL) kupitia kampuni ya wakala wa ukatishaji tiketi ya Salama World Travel iliyopo visiwa vya Comoro.
Hii ni moja ya harakati za serikali kulifufua Shirika la Ndege Tanzania.
Kufuatia upotevu huo wa fedha, mkurugenzi wa Fedha wa ATCL Steven Kasubi amesimamishwa kazi.
Image captionShirika la ndege la Air Tanzania
Uchunguzi umeanza chini ya kikosi cha polisi kitengo cha usalama mitandaoni ili kubaini mtandao mzima wa wote walivyohusika

Tuesday, February 9, 2016

BIDHAA ZILIZOPITWA NA MUDA WAKE ZAPIGWA MARUFUKU KUTUMIKA




 
Mfanyabiashara wa duka la rejareja B.Mariam kilusu akielezea kuhusiana na biashara yake anayoifanya

Mama huyu amesema  bidhaa zote ni nzuri isipokuwa jambo kubwa ni kuzingatia kuangalia ubora wa bidhaa ili kuepuka kuwauzia wateja vitu ambavyo vimepitwa na muda wake.

Bidhaa bora zinatambulika pale unaponunua kwani unageuza upande wa ganda au karatasi iliyobandikwa ili kuona muda wa bidhaa ile kuiosha muda wake.

BIDHAA ZINAZODUMU

 
Baadhi ya bidhaa zinazodumu madukani bila kupitwa na mda wake.

Hizi ni zile bidhaa ambazo mara nyingi hazipitwi na mda wake lakini pia nyingine huuzika kwa wepesi zaidi,

Aina ya bidhaa sinazouzika kwa urahisi ni kama maji.bidhaa hii haichukui muda mrefu kukaa dukani  kwani huwa ni hitaji muhimu kwa binadamu kwa mahitaji ya kila siku.

Bithaa nyingine zinazodumu bila{ kuexpire}kupitwa na muda wake ni kama uzi taa za umeme n.k

BAADHI YA BIDHAA ZIPATIKANAZO KWENYE MADUKA YA REJAREJA NCHINI




 Katika picha ni aina mbalimbali za bidhaa zinazopatikana kwenye maduka ya rejareja nchini ambazo mara nyingi hupitwa na muda wake

Wafanya biashara wa maduka ya rejareja  nchini wameshauriwa kuchukua bidhaa  zinazoendana na mauzo yao ili kuepuka kuuza bidhaa zilizopitwa na muda wake{expire}.

Hayo yamesemwa nammoja wa wafanyabiashara wa maduka ya rejareja B.Marium kilusu wakati akiongea na AJTC Redio katika mtaa wa kwa Morombo jijini Arusha, akielezea changamoto wanazokumbana nazo katika biashara hiyo.

Amesema uuzaji wa bidhaa zilizoisha muda wake imekuwa tatizo kubwa kwa watanzania kitu ambacho husababisha baadhi ya maduka kuzorota kutokana kwamba mteja atakayebeba bidhaa hatarud tena akifikiri bithaa zote ni sawa.

Hata hivyo ameongeza kuwa bidhaa mbovu huleta madhara kwa watumiaji kutokana na matumizi ya bidhaa husika kama sabuni ,mafuta,na vinywaji .

‘’sisi wauzaji tunatakiwa tuwe makini wakati wa kwenda kufungasha mzigo tuhakikishe tunachukua bidhaa ambazo hazijaharibika au ambazo haziharibiki haraka kulingana na aina ya wateja wetu tuwapende tuwatunze ili kuweza kuendeleza soko letu bila vikwazo vyovyote kutokea’’

Baathi ya wananchi wa jijini Arusha wameiomba serikali kukagua maduka yenye bidhaa zilizopitwa na wakati ili kuwasaidia watu wasiojua kutambua / kusoma au kuona kuwa ipi ni nzuri {updated}.


BAADHI YA BIDHAA AMBAZO ZINAHITAJI UMAKINI KATIKA KUANGALIA MDA WAKE {EXPIRE DATE}


Hizi ni baadhi ya bidhaa ambazo asilimia kubwa ya wananchi hutumia sana pasipo kuangalia kuwa 
zinamaliza lini mda wake wa matumizi.

Baathi ya bidhaa kama tomato sabuni za unga na nyinginezo humaliza mda kwa kukaa sana dukani .