Mhungaji wa kanisa la Timotheo tawi la TAG lililopo kwa morombo jijini arusha Bw. Raimond Matwi.
Wakristo wote nchini
wameaswa kutenda matendo
yaliyomema maana mwokozi wa
ulimwengu yesu kristo amezaliwa kwa
ajili yao.
Kauli hiyo imetolewa
hivi karibuni na mchungaji wa kanisa la Timotheo lililo kuwa Arusha mjini mchungaji Raimond amewaasa wakristo wote kumrudia mungu kwa kutenda matendo yaliyo mema.
Sanjari na hayo amewaomba kusherekea kwa amani na utulivu na kumtaka kila mtu ampende jilani
yake kama anavyo jipenda mwenyewe na amsaidie mavazi na chakula pale panapo
wezekana nakusema huo ndio ukristo.
Mchungaji Raimond amewataka wakristo waache kuwa watumwa wa zambi na kuwataka wahudhurie
katika nyumba za ibada ili kufurahia
ujio wa bwana wetu yesu kristo
.
Pia mchungaji huyo ameipongeza serikali ya awamu ya tano
kwa namna inavyofanya kazi kwa
bidii na kuwaombea aendelee kuwapa nguvu
za kufanya kazi kwa bidii
.
Vilevile amelishukuru jeshi la polisi kwa kuendelea kuweka
ulinzi na usalama katika mkoa wa
Arusha hasa katika kipindi hiki cha
kwaresma.
No comments:
Post a Comment