Wafanyabiashara wa soko la kwa Morombo wagoma kuhama
Mwenekiti wa mtaa wa FFU Bw Anaclet Edward
Bi. Regina Makorongo akichochea moto
Mfanyabiashara wa soko la kwa morombo jijini Arusha Zena Shabaan
Wafanyabiashara wa soko la kwa Morombo wamegomea manispaa ya
jiji la Arusha kuhamimia katika eneo lililotengwa na serikali na kusema hawako
tayari kutokana na miundo mbinu ya soko hilo kuwa mibovu na kuhofia usalama wa mali zao
Hata hivyo amesema kuwa mtu anapokamatwa na manispaa
anatakiwa apelekwe mahakamani na siyo mahali pengine na kuiomba serikali hii ya awamu ya tano iwatengenezee mazingira
mazuri ya biashara
“Yaani hawa manispaa wanatunyanyasa kwa kweli, sisi kufanya
biashara zetu pembezoni mwa barabara ni kutokana na mazingira ya soko ambalo
walitupeleka kuwa mibovu na hakuna ulinzi wowote ambao utaweka hali ya usalama
tunalipa kodi sasa hizo pesa zetu za kodi wanazipeleka wapi ?” Alisema mmoja wa
wafanyabiashara
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa FFU
ambako linapatikanaa soko hilo Bw. Anaclet Edward amesema kuwa eneo wanalofanyia biashara kwa sasa ni
kinyume cha sheria kwani mwaka jana
walipewa barua ya maandishi wahame eneo hilo lakini cha kushangaza hadi sasa
wapo wanaendelea na biashara
Sanjari na hayo Bw. Edward ameongeza kwa kusema yeye
hawanyanyasi wananchi wake bali
anatekeleza jukumu hilo kwa manufaa yao wenyewe
“Mimi nafanya hivyo kwa ajili ya kuwaweka kwenye usalama kwa
siyo tu ni amri kutoka manispaa ya jiji letu hili cha msingi wananchi wafuate
kanuni na utaratibu unavyotaka”Aliongea
mwenyekiti huyo
No comments:
Post a Comment