Tuesday, March 1, 2016

WANANCHI WAMEOMBWA KUTUNZA MIUNDO MBINU

Wito umetolewa kwa wakazi  wa mkoa   wa Arusha  kutunza miundombinu ili kujikinga  na mvua nyingi zinazoendelea  kunyesha hasa  kipindi hiki cha masika
.
Hayo yamesemwa  hivi   karibuni na mamlaka ya hali ya hewa hivi karibuni   na mamlaka ya hali ya hewa Tanzania  ili kuweza kutoa  tahadhari kwa wananchi kwani mvua zinazoendelea kunyesha huenda zikaleta madhara  makubwa ndani ya nchi.

 Tahadhari hiyo ya mamlaka ya hali ya hewa Tanzania[TMA]  imewasisitiza  wenyekiti wa  serikali za mitaa  Mkoani Arusha ambapo wamewaomba  viongozi kutoka halmashauri  ya mkoa  kutembelea kata  hizo ili  kujionea  hali ya miundombinu.


 Mbali na hayo  wamesema hawatalifumbia macho agizo la mamlaka ya hewa Tanzania kwani mvua  imekuwa nyingi  na inaendelea kuleta madhara katika baadhi ya kata

.

No comments:

Post a Comment