Wednesday, April 13, 2016

Rais Magufuli aongoza mamia kumuaga mbunge mstaafu


Rais John Magufuli akiaga mwili aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalum wa Chadema, Christina Lissu Mughwai katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam jana. ( Picha na Ikulu).

RAIS John Magufuli ameungana na mamia ya waombolezaji kuaga mwili wa Mbunge mstaafu wa Mkoa wa Singida, Marehemu Christina Lissu Mughwai katika ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es Salaam.

Mughwai aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida katika kipindi cha kuanzia mwaka 2010 hadi 2015, aliagwa jana kabla ya kusafirishwa kwenda kijiji cha Mahambe mkoani Singida kwa maziko.

Pamoja na Rais Magufuli na mkewe Mama Janeth, viongozi wengine waliohudhuria shughuli ya kuaga ni Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Akson na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bunge, Freeman Mbowe.

Akitoa salamu kwa niaba ya Rais Magufuli, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene aliwapa pole familia ya marehemu. Alisema katika kipindi chake cha ubunge, Mughwai alitoa mchango mkubwa kama mbunge na kama mtaalamu wa Uchumi

No comments:

Post a Comment