Wanafunzi wakisikiliza semina
Bi Fatma Amiry akitoa semina ya jinsia katika ukumbi wa chuo cha uandishi wa habari Arusha
Kulingana na usanyanyasaji wa kijinsia
unaoendelea katika maeneo
mbalimbali nchini,jamii imehaswa
kuweka usawa wa kijinsia ili kuweza kutokomeza adha hiyo.
Hayo yamesemwa na Bi. Fatma Amiry ambaye ni Afisa ustawi wa
jamii mkoani Arusha katika semina ya
kupinga unyanyasaji wa kijinsia
na maambukizi ya Ukimwi iliyofanyika katika ukummbi wa chuo cha Uandishi wa
Habari na utangazaji Arusha (AJTC).
Ameeleza kuwa jamii nyingi za kitanzania bado zinamitazamo hasi kuhusiana na suala la usawa wa kijinsia
kutokana na mila na destuuri walizojiwekea ambazo zinaleta migogoro na usnyanyasaji wa kijinsia.
Bi Fatma amesema jamii inatakiwa ibadilike kulingana na wakati
uliopo ili kuweza kuleta usawa huo katika jamii ikiwa ni pamoja na wanawake
kurithi mali,kupewa elimu na kutokudharauliwa
“Ni wakati wa
mabadiliko katika jamii zetu, maisha ya zamani ni tofauti na sasa hivyo
nawaomba watanzania wenzangu waache kunyanyasa jinsia tofauti ili kuweza
kutimiza malengo ya haki sawa kwa wote”Alisema Bi. Fatma Amiry
Licha ya hayo pia amewashauri
vijana na jamii kwa ujumla kupima
afya na kuwa waaminifu kwa wapenzi wao ili kuweza kupunguza kasi ya maambukizi ya virus vya Ukimwi
Kwa
upande wake mkufunzi wa chuo hicho Bw. Lucas Modaha amesema vijana na wanandoa wajiheshimu na kulinda utu
ili kuepuka maambukizi mapya ya VVU
No comments:
Post a Comment