Monday, February 29, 2016

TCRA YAZIPIGA FAINI E FM NA KAHAMA FM

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandili ya TCRA, Margaret Munyagi

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imevipa onyo na kuvipiga faini vituo viwili vya redio kutokana na kukiuka maadili ya utangazaji.

Vituo hivyo ni Entertainment FM (E FM) cha Dar es Salaam na Kahama FM Stereo ya Kahama, mkoani Shinyanga
.
Akitoa maamuzi yaliyofikiwa na Kamati ya Maandili ya TCRA, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Margaret Munyagi, alisema vituo hivyo vimebainika kukiuka sheria na kanuni za utangazaji.
Amevitaka viwe na usimamizi mzuri wa vipindi vyao.

Munyagi alisema kamati yake imekipa onyo kali na faini ya sh milioni moja kituo cha Efm na endapo kitarudia, hatua kali zaidi zitachukuliwa
.
Alisema Januari 4 mwaka huu, kituo hicho katika kipindi cha ‘Joto la Asubuhi’ katika kipengele cha ‘Sala ya Siku’, kilichorushwa kati ya saa 1 hadi 3 asubuhi, Mtangazaji alihamasisha vitendo vya wizi, ngono na uchochezi wa kidini
.
Katika utetezi wake, Mkurugenzi wa kituo hicho, Dennis Busulwa pamoja na kukiri kufanya kosa, alisema kituo chake kilijibebesha mzigo mzito wakati bado ni wachanga katika utangazaji na kutokana na kosa hilo waliamua kukiondoa kipengele hicho
.
Kwa upande wa Kahama FM Stereo, Munyagi alisema kituo hicho kimepewa onyo kali, kutozwa faini ya Sh 200,000 na endapo watajirudia watapewa adhabu kali.

Januari Mosi mwaka huu, kupitia kipindi cha ‘Wanawake’ kilichorushwa hewani kati ya saa 3 asubuhi na saa sita mchana, mtangazaji alimhoji mwanamke aliyekuwa akifanya biashara ya kujiuza.

“Mahojiano hayo yalijikita katika kuelezea jinsi biashara ya kujiuza inavyofanyika katika mji wa Kahama kwa kubainisha changamoto na faida ambazo wafanyabiashara hiyo wanazipata. “Kuwepo kwa majadiliano haya katika muda wa asubuhi kunaweza kuchochea tabia mbaya kwa watoto kuiga vitendo vya ufanyaji ngono,” alisema.

Katika utetezi wake, Meneja wa Kahama FM Stereo, Marco Mipawa, alikiri kikiuka sheria na kanuni za utangazaji na kuahidi kwamba tatizo hilo halitajirudia tena.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO AZITAKA TEMESA, TBA NA NCC KUFANYA KAZI KWA UADILIFU


Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani akiongea na menejimenti ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) alipowatembelea katika ofisi zao leo jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya kuzitambua taasisi zilizopo chini ya wizara yake.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani akiongea wakati wa kikao na wafanyakazi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) alipowatembelea katika ofisi zao leo jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya kuzitambua tasisi zilizopo chini ya wizara yake kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa TBA Arch.Elius Mwakalinga.
Wafanyakazi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani (hayupo katika picha) leo jijini Dar es Salaam, katika ziara ya kuzitambua tasisi zilizopo chini ya wizara yake.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani akimsikiliza Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi. Manase Ole Kujan katika ziara yake ya kuzitambua tasisi zilizo chini ya wizara yake kwa kuangalia majukumu yanayotekelezwa na Taasisi hizo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani (Kushoto) akifafanua jambo kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) Mhandisi.Julius Mamilo(kulia) wakati ziara yake ya kuzitambua tasisi zilizo chini ya wizara yake kwa kuangalia majukumu yanayotekelezwa na Taasisi hizo leo jinini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani(Hayupo katika picha) Mamilo katika ziara yake ya kuzitambua tasisi zilizo chini ya wizara yake kwa kuangalia majukumu yanayotekelezwa na Taasisi hizo leo jinini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani, amezitaka taasisi zilizo chini ya Wizara yake kufanya kazi kwa uadilifu, bidii na kwa uharaka ili kuendana na kasi ya madiliko ya Serikali ya awamu ya Tano.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam, wakati alipofanya ziara katika taasisi zilizo chini ya Wizara yake ikiwemo Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) kwa lengo la kupata mafunzo ya kiutendaji katika taasisi hizo.

Aidha amezitaka taasisi hizo kuongeza ukusanyaji wa mapato katika vyanzo vya mapato walivyonavyo na kamwe kutotegemea ruzuku kutoka Serikalini.

“Nataka ifikapo mwaka wa fedha ujao makusanyo ya mapato yawe yameongezeka zaidi kuliko matumizi na kamwe msikae kusubiri ruzuku kutoka Serikalini, kikubwa ni kubuni vyanzo vyengine vya mapato ili kuweza kujiendesha”, alisema Naibu Waziri.

Hata hivyo Naibu Waziri huyo amewataka watendaji hao kufanya kazi kwa weledi na bila woga kwani Serikali haitamuonea huruma yeyote anayekiuka kutekeleza wajibu wake.

“Nawaomba mfanye kazi kwa morali kubwa ili kuweza kuisaidia jamii ambayo inahitaji huduma muhimu kutoka Serikalini”, alifafanua Eng. Ngonyani.

Katika hatua nyingine Eng. Ngonyani amemtaka Kaimu Mtendaji Mkuu wa TEMESA Eng. Manase Ole kujan kutatua changamoto walizonazo ili kuleta mabadiliko chanya katika taasisi hiyo.

“Una nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko hasa katika mfumo mzima wa ukatikatishaji tiketi eneo la Magogoni ambalo limekuwa kero katika mfumo mzima wa ukusanyaji wa mapato”, alisisitiza Naibu Waziri Ngonyani.

Sambamba na hilo Naibu Waziri amemtaka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania Arch. Elius Mwakalinga, kuandaa taarifa ambayo itaonyesha idadi ya nyumba za Serikali wanazomiliki na ibainishe taarifa ya watumishi wenye stahili ya kupangishwa kwenye nyumba hizo.

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa TEMESA Eng. Manase Ole Kujan amesema wakala huo umepanga kuboresha miundombinu hasa katika usafiri wa majini na kuhakikisha inapunguza changamoto ya usafiri katika vivuko.

Naye Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi, Eng. Julius Mamilo amebainisha changamoto walizonazo ikiwemo uhaba wa fedha hali inayosababisha Baraza hilo kukwama katika kufanya kazi katika miradi yake ya maendeleo hususan katika kufanya kazi za utafiti

Sunday, February 28, 2016

Ufisadi wa vitabu waathiri darasa la kwanza



Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Teknolojia, Sayansi na Ufundi, Maimuna Tarishi akitoa tamko la Serikali la kuwasimamisha kazi baadhi ya watumishi wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) baada ya kushindwa kutekeleza maagizo ya kusitisha uchapaji wa vitabu vya kiada kwa darasa la kwanza ambavyo vilikuwa na kasoro. Mwingine ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Leonard Akwilapo. (Picha na Fadhili Akida).

UFISADI uliofanyika katika uchapaji wa vitabu 2,807,600, vilivyo tayari kutumika kwa ajili ya darasa la kwanza nchi nzima, umesababisha wanafunzi hao, ambao mwaka huu udahili wao umeweka historia kwa idadi kubwa kuwahi kudahiliwa, kulazimika kutumia vitabu vya zamani.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Maimuna Tarishi (pichani), alisema hayo jana alipokutana na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam. Alifafanua kwamba kasoro kubwa, zilizobainika katika vitabu hivyo, ambavyo vilishafika katika ghala la Serikali, zimesababisha Serikali izuie visisambazwe.
Kwa mujibu wa Tarishi, vitabu hivyo vya ‘Najifunza Kusoma Kitabu cha Kwanza’ na ‘Najifunza Kusoma Kitabu cha Pili’, vimechapwa na kampuni ya Yukos Enterprises, ambayo ni moja ya kampuni tatu zilizoshinda zabuni ya kazi hiyo iliyotangazwa Aprili mwaka jana.
Lakini, alisema kasoro hizo zimesababisha Serikali kuagiza viondolewe katika ghala lake na udhibiti ufanyike visisambazwe mashuleni.
Upungufu
Kasoro zilizokutwa ni muingiliano wa rangi, upungufu wa kurasa, picha moja kuwa na rangi tofauti, ukataji usiozingatia vipimo, baadhi ya vitabu kufungwa kwa pini moja katikati badala ya mbili, huku vingine vikikosa pini kabisa na vingine vikifungwa ubavuni.
Kasoro nyingine ni vingine vimekutwa vimechakaa kabla ya matumizi, hasa kitabu cha ‘Najifunza Kusoma Darasa la Kwanza Kitabu cha Pili’; vingine vikiwa na mpangilio mbaya wa kurasa, ufifiaji wa maandishi huku picha katika baadhi ya vitabu na maandishi, vikishindwa kuonekana kabisa.
Kasoro nyingine kwa mujibu wa Tarishi ni namba za kurasa kutoonekana kabisa, baadhi ya kurasa kujirudiarudia, baadhi ya kurasa kutotenganishwa, maandishi ya baadhi ya vitabu kugeuzwa mwelekeo, majalada kuwa zaidi ya moja na baadhi ya vitabu kukutwa vimedurufiwa (photocopy).
Katibu Mkuu huyo alisema kasoro hizo, zilibainika baada ya ufuatiliaji kufanywa na Wizara katika bohari iliyokuwa ikipokea vitabu hivyo.
“Kutokana na kasoro hizo, ni dhahiri mchapaji Yukos Enterprises Ltd hakuzingatia vigezo vilivyowekwa na kwa kufanya hivyo amekiuka makubaliano yaliyo katika mkataba alioingia na Taasisi ya Elimu Tanzania,” alisema Tarishi.
Athari zake
Kutokana na hali hiyo, Tarishi alisema wanafunzi wa darasa la kwanza mwaka huu watapungukiwa vitabu vya kujifunza kusoma, kwa kuwa haviwezi kutumika. Hivyo aliagiza wanafunzi wa darasa la kwanza mwaka huu, watumie vitabu vya zamani na walimu watatumia ‘Kitabu cha Kiongozi cha Mwalimu’ ambacho ni kipya.
Kuhusu gharama iliyotumika, Tarishi alisema ni zaidi ya Sh bilioni mbili, lakini alibainisha kuwa mchapishaji alikuwa amelipwa asilimia 20 tu kwa kutumia dhamana ya benki.
Majipu yatumbuliwa
Kasoro hizo zimemlazimu Katibu Mkuu huyo kuagiza Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), kuwasimamisha kazi vigogo wa taasisi hiyo, akiwemo Kaimu Mkurugenzi Idara ya Vifaa vya Kielimu, Peter Bandio, Mwanasheria, Pili Magongo na Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi na Ugavi, Jackson Mwaigonela.
Hatua hiyo imetakiwa kufuatia uchunguzi katika taasisi hiyo, kuhusu vipi wameshindwa kusimamia Sheria ya Manunuzi na kazi ya uchapaji wa vitabu.

NDOA ZA UTOTONI ZAPIGWA MARUFUKU NCHINI



Afisa  ustawi wa jamii Bw. Shija Numbu




Wazazi na walezi nchini wameaswa kuheshimu  haki za watoto na kujua kwamba suala la kuhudumia watoto sio hiari ya mtu bali ni lazima kwa mujibu wa sheria.

Hayo yamesemwa na   Afisa wa ustawi wa jamii wa jiji la Arusha Mr Shija Numbu wakati akiongea na mgonja blog  ofisini kwake.

Amesem  baadhi ya jamii za kiafrika humnyima mtoto haki yake kwani mtoto hutolewa mahari akiwa tumboni mwa mama yake hali ambayo humpelekea baadae kuolewa akiwa na umri mdogo lakini pia kuolewa na mtu ambaye  pengine hajampenda.

''Kesi za  ndoa za utotoni  tunazipokea hapa kwa sababu ya mila za kimaasai kwamba mtu anatolewa mahari akiwa tumboni  akizaliwa wa kike  akifikisha miaka saba[7 ] akachukua mke wake  baadae ustawi wa jamii  wakajua na kuweza kufuatilia  suala hili''

Kwa kuzingatia sheria  ya haki ya mtoto.ya  mwaka 2009 amesema mtoto ana haki ya kukaa na wazazi wake mpaka pale atakapotimiza umri wa miaka kumi na nane [18] na kuendelea .

Ameongeza kuwa watoto wote wana haki sawa  kwani kila mtoto ana haki ya kupata kila aina ya hitaji atakalohitaji.

Mr shija amesema  watoto wote wana haki sawa katika katika suala zima la  ndoa za utotoni kwani vipo vipengele vinavyomlinda mtoto wa  kike lakini pia vipo vya kumlinda mtoto wa kike.

''Sheria ya mwaka 2008  mtoto chini ya umri  wa miaka 18hairuhisiwi kuolewa kwani ni sawa na ubakaji, na kwa upande wa mtoto wa  kiume  sheria inasema hajabaka bali kamnyonya mtoto kingono.


Thursday, February 25, 2016

Chuo Kikuu St. Joseph wagoma



Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Yunus Mgaya
 
WANAFUNZI 1,548 wa Chuo Kikuu cha St. Joseph tawi la Arusha, wamegoma kuingia darasani kwa siku tatu na kukodi mabasi matatu kwenda Dar es Salaam kumwona Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.
Lengo la safari yao hiyo ya Dar ni kujua hatma yao, baada ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), kufungia chuo hicho tawi la Songea.
Hata hivyo, Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Yunus Mgaya, alibainisha kuwa hatma ya chuo hicho, itatolewa rasmi kesho baada ya tume hiyo kupitia mapendekezo ya tume ya wataalamu iliyoundwa mapema kwa ajili ya ukaguzi wa chuo hicho, tawi la Arusha.

Kulikuwa na vurugu miongoni mwa wanafunzi juzi jioni, hali iliyofanya uongozi kufikia uamuzi wa kufunga chuo hicho kwa muda usiojulikana. Wakizungumza jana kabla ya kuanza safari kwenda Dar es Salaam kumwona Waziri Ndalichako, wanafunzi hao walisema mmiliki wa St. Joseph ni mmoja, hivyo kama tawi la Songea lina shida ni wazi matawi yote nchini yana shida.

Waliomba serikali kutoa ufafanuzi, kabla ya kuendelea kupoteza fedha za umma walizopatiwa kama mikopo.

“Pamoja na Tume ya Vyuo Vikuu kutoa waraka kwenye mtandao kuwa kufungwa kwa chuo cha Songea, hakuhusiani na matawi ya chuo hicho, lakini sisi hatuna hakika tunataka watu hakikishie kama tupo salama,” alisema mwanafunzi Joel Lameck.

Aliendelea kusema, “na tukimaliza masomo yetu, je, tutapata ajira serikalini, yasije yakatukuta ya Chuo cha St. John cha Dodoma ambao hawakupata ajira kwa sababu elimu waliyopata haikuwa na viwango.

Wanafunzi hao ambao wengi wao hawakutaka majina yao yatajwe gazetini, walisema wamekuwa wakilalamika mara kwa mara kuwa chuo hicho kina upungufu mwingi, ikiwemo uhaba wa vifaa vya kufundishia.

Pia wanafunzi hao walihoji sababu za serikali, kutowaleta wanafunzi wa tawi la Songea iwapo tawi lao la Arusha lipo salama, badala yake wamepelekwa vyuo vingine, nje ya St Joseph.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Siles Balasingh, aliomba serikali kutoa majibu haraka kwa wanafunzi hao wanaosomea ualimu wa masomo ya Sayansi, waendelee na masomo yao, kwani wamepata wasiwasi baada ya kufungwa tawi la Songea, japo hawana shida na chuo.

Alisema wao kama chuo, wamejitahidi kubandika chuoni hapo tangazo la TCU kwamba tawi hilo halihusiki na matawi mengine, lakini wanafunzi hawaelewi, wamegoma kuingia darasani, pia wameharibu mali za chuo.

“Hawa wanafunzi leo siku tatu hawataki kuingia darasani na wamekodi mabasi matatu wanaelekea Dar es Salaam kumwona waziri, lakini wamewapiga baadhi ya wanafunzi wenzao kwa kuwakataza kufanya mitihani mpaka wapate uhakika wa masomo tunayowapatia kama tumekidhi vigezo vya mitaala ya elimu,” alisema
.
Alisema walimu wanasikitika kuona vurugu zinatokea kwa sababu hiyo, hivyo ikiwezekana wanamwomba waziri wa elimu afike chuoni hapo, kutoa ufafanuzi ili wanafunzi wao hao wapatao 1,518 waendelee na masomo yao.

Hatma ya chuo kujulikana Ijumaa
Akihojiwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dar es Salaam jana, Profesa Mgaya alisema mgogoro wa chuo hicho, ulianza muda mrefu tangu mwaka 2014, hali iliyosababisha tume hiyo kufanya ukaguzi chuoni hapo.

“Tume iliunda timu ya wakaguzi iliyoongozwa na maprofesa wa taaluma mbalimbali, waliokagua mfumo wa ufundishaji, mazingira ya ufundishaji na kuhoji wanafunzi chuoni hapo. Tayari timu hii imewasilisha ripoti yake kwa TCU,” alisisitiza.

Alisema leo tume hiyo inatarajia kukutana na timu hiyo na Kamati ya Ithibati majira ya saa 3 asubuhi, kuijadili ripoti ya ukaguzi wa chuo hicho na saa 9 mchana itaitisha mkutano wa dharura kujadili mapendekezo ya taarifa hiyo na kutoa maamuzi dhidi ya chuo hicho.

“Tutautangazia umma Ijumaa (kesho) majira ya saa nne asubuhi kuhusu hatma ya chuo hiki cha St Joseph tawi la Arusha.

Wanafunzi waliochochea wenzao wajisalimisha India




Image caption

Wanafunzi wawili wa kihindi waliodaiwa kuwachochea wanafunzi wa chuo kikuu cha Jawaharlal Nehru kuandamana huko Delhi wamejisalimisha kwa polisi wenyewe.
Umar Khalid na Anirban Bhattacharya ni miongoni mwa wale waliokuwa wakitafutwa na polisi.
Kukamatwa kwa kiongozi wa muungano wa wanafunzi wa chuo hicho Kanhaiya Kumar, mapema mwezi huu ndiko kulikosababisha ghasia katika sehemu nyingi nchini India.
Baada ya Bwana Kumar kukamatwa, wanafunzi wengine ambao wametajwa kuhusiana na maandamano hayo walitoweka lakini wakajitokeza katika chuo kikuuu cha JNU siku ya Jumapili usiku.
Polisi hawakuingia katika chuo hicho lakini jumanne usiku Umar Khalid na Anirban Bhattacharya waliondoka katika chuo hicho kwa hiari na kujisalimisha kwa polisi.
Polisi hawaruhusiwi kuingia vyuoni bila idhini ya viongozi wa chuo,ripoti zimesema.
Polisi wamewata wanafunzi waliosalia - Ashutosh Kumar,Anant Prakash Narayan, Riyazul Haq na Rama Naga -kujisalimisha

NICE MEDIA PRODUCTION KWA MAFANIKIO ZAID

KWA PAMOJA TUSHIRIKIANE KUMSIFU MUNGU KWA KUSIKILIZA WIMBO HUU UNAOJULIKANA KWA JINA LA NAJIVUNIA KUWA NA YESU,AMBAO UMEFANYIKIA KATIKA STUDIO YA NICE MEDIA PRODUCTION ILIYOPO JIJINI ARUSHA.

TUSHIRIKIANE KUWALINDA ALBINO NA WAZEE

SHIRIKIANA NASI KUSIKILIZA WIBBO HUU KWA AJILI YA KUWATUNZA NA KUWATHAMINI WENZETU WENYE ULEMAVU WA NGOZI.WIMBO HUU UMEIMBWA NA MWIMBAJI MR$ MRS ELIHURUMA CHAO KATIKA STUDIO YA NICE MEDIA.

Wednesday, February 24, 2016

BESIGYE; NILIKAMATWA MARA NNE


Image copyrightAP
Image captionKiongozi wa Upinzani wa Chama cha FDC, Kizza Besigye

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kiiza Besigye ameiambia BBC Kuwa ametiwa mbaroni na polisi mara nne kwa muda wa siku sita kufuatia uchaguzi uliofanyika nchini humo wiki iliyopita. Matokeo ya uchaguzi huo yalimpa ushindi Rais Yoweri Museven kutawala nchi hiyo kwa muhula wa tano.
Bwana Besigye ambaye yupo kizuizini nyumbani kwake ameeleza jinsi alivyokamatwa na polisi.
"nilikamatwa na polisi nikiwa nyumbani mwendo wa saa kumi na moja alfajiri, na kupelekwa kwa mwendo kasi mjini ambao ulikuwa ni mwendo wa kutisha ili kuwakwepa waandishi wa habari waliokuwepo katika eneo walinikamata, na hii ilkawa ni mara ya nne kukamatwa na polisi kwa muda wa siku sita."
Besigye amesema amesikitishwa sana kwamba jamii ya kimataifa haijaingilia kati suala hilo kwa niaba yake. Ameonya kwamba kama wanadhani Rais Museveni ameleta amani na utulivu nchini Uganda wajue wanafanya makosa.
"Amani na utulivu ni upande mmoja wa sarafu. Upande wa pili wa sarafu ni haki. Hauwezi kuwa na amani na utulivu bila haki. Na hii ndio hali halisi katika mazingira yetu ni kwamba kwa kifupi hakuna haki "alieleza

WANAFUNZI WALIOCHOCHEA WENZAO WAJISALIMISHA HUKO INDIA



Image captionMwanafunzi aliyewachochea wenziwe India
Wanafunzi wawili wa kihindi waliodaiwa kuwachochea wanafunzi wa chuo kikuu cha Jawaharlal Nehru kuandamana huko Delhi wamejisalimisha kwa polisi wenyewe.
Umar Khalid na Anirban Bhattacharya ni miongoni mwa wale waliokuwa wakitafutwa na polisi.
Kukamatwa kwa kiongozi wa muungano wa wanafunzi wa chuo hicho Kanhaiya Kumar, mapema mwezi huu ndiko kulikosababisha ghasia katika sehemu nyingi nchini India.
Baada ya Bwana Kumar kukamatwa, wanafunzi wengine ambao wametajwa kuhusiana na maandamano hayo walitoweka lakini wakajitokeza katika chuo kikuuu cha JNU siku ya Jumapili usiku.
Polisi hawakuingia katika chuo hicho lakini jumanne usiku Umar Khalid na Anirban Bhattacharya waliondoka katika chuo hicho kwa hiari na kujisalimisha kwa polisi.
Polisi hawaruhusiwi kuingia vyuoni bila idhini ya viongozi wa chuo,ripoti zimesema.
Polisi wamewata wanafunzi waliosalia - Ashutosh Kumar,Anant Prakash Narayan, Riyazul Haq na Rama Naga -kujisalimisha

Tuesday, February 23, 2016

MAKAMPUNI NA TAASISI BINAFSI NCHI ZIMEASWA KUIMARISHA AMANI NA ULINZI.

 Taasisi na makampuni binafsi nchini wameaswa kuboresha  na kuimarisha  ulinzi kwa lengo la kujihami  na maadui wanaojitokeza.


     Bandari  iliopo jijini tanga

Hayo yamesemwa na Kamanda  wa polisi wa polisi jiji la Arusha Bw. Liberatus Sabas wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
     Kamanda wa polisi mkoani Arusha  Bw. Liberatus Sabas


Hata hivyo amewasisitiza wamiliki wa taasisi na makampuni binafsi kuweka ulinzi wa kutosha  na wenye uhakika na kuchukua na kuchukua walinzi kutoka kwenye makampuni ya ulinzi yenye vitendea kazi vya kisasa.

Vilevile amewataka wananchi kutoa taarifa mapema hasa zile wanazozitilia mashaka  kwa ajili ya kulinda na kuboresha amani.

Pia  amewaasa wananchi  kujichukulia  sheria mkononi kwani zinajaribu kupata mtandao mzma wa kuharifu na kuwataka watoe taarifa katika vyombo vya habari nchini.

Nao baadhi ya wamiliki wa hoteli jijini Arusha Bw. Saimoni Mrema na Bw. Vanley Gopal wamelishukuru jeshi la polisi  kwa kuimarisha ulinzi katika  viunga  hapa jijini Arusha  na kuwahakikishia utakuwa wakutosha. 

TRA YAKUSANYA KWA MWEZI TRILION1.7




SERIKALI imeendelea kupaa katika ukusanyaji wa mapato baada ya kukusanya hadi Sh trilioni 1.79, ambazo imezipeleka katika huduma za jamii, ikiwamo elimu, maji, miundombinu na miradi ya maendeleo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Servacius Likwelile alisema hayo jana wakati akitoa taarifa ya hali ya mapato kwa kipindi cha Februari mwaka huu. Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata alisema makusanyo yameongeza kutoka Sh trilioni 1.2 Desemba hadi Sh trilioni 1.79 Januari.
Kabla ya Oktoba mwaka jana, makusanyo hayo hayakuzidi Sh bilioni 900 kwa mwezi. Dk Likwelile alitaja maeneo ambayo fedha hizo zimeelekezwa ni kwa Mamlaka ya Elimu (TEA) iliyopewa Sh bilioni 23.078; Sh bilioni 18.7 zinatekeleza utoaji wa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za awali, msingi hadi kidato cha nne kwa ajili ya ada, chakula na ruzuku.
Aidha, Sh bilioni 13 zimeelekezwa kwenye mikopo ya elimu ya juu na Sh bilioni moja zitatumika kujengea uwezo walimu walio masomoni na wakufunzi wao. Pia Sh bilioni mbili zimeelekezwa kupanua udahili katika mkoa wa Dar es Salaam kama Rais John Magufuli alivyoahidi katika mkutano wake na wazee wa mkoa huo.
Dk Likwelile alitaja maeneo mengine yaliyonufaika na fedha hizo na shilingi kwenye mabano ni Mpango wa Maji Vijijini (bilioni 17.1), maendeleo ya ujenzi wa barabara (bilioni 58.8), miradi ya umeme vijijini (bilioni 20.2), reli (bilioni 2.034) Serikali za Mitaa (bilioni 4.5), na Mahakama zimepatiwa Sh bilioni 12.3.
Wakati huo huo imeelezwa kuwa makusanyo yameongeza kutoka Sh trilioni 1.2 Desemba hadi Sh trilioni 1.79 Januari.
Kabla ya Oktoba mwaka jana, makusanyo hayo hayakuzidi Sh bilioni 900 kwa mwezi. Aidha, Dk Likwelile alisema ili kuwajengea uwezo walimu walio masomoni na wakufunzi wao, Wizara imetoa Sh bilioni 1.65 kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.
Kati ya fedha hizo, wakufunzi wamepatiwa Sh milioni 431.6, walimu walio masomoni wametengewa Sh milioni 249.2 kwa ajili ya vifaa vya kufundishia, posho na nauli.
Alisema kuwa fedha nyingine kati ya hizo, kiasi cha Sh bilioni 573.7 zimetolewa kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa umma na ulipaji wa deni la taifa kwa mwezi huu zimetolewa Sh bilioni 842.1 na mifuko ya hifadhi za jamii Sh bilioni 81.13.
Aidha kiasi kilichotolewa kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo ni Sh bilioni 166.2 huku Chuo kipya cha Sayansi ya Tiba kilicho katika hatua ya ujenzi cha Mloganzila huko Kibamba, nje ya Jiji la Dar es Salaam, kimepatiwa Sh bilioni 18

Bilioni 4/- zaokolewa kwa kuzuia safari


Waziri, Ofisi ya Rais, Tamisemi, George Simbachawene
OFISI ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imeokoa Sh bilioni 4.38 ambazo zingetumika na watumishi wa Halmashauri mbalimbali nchini kwa ajili ya safari za ndani.
Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene alibainisha hayo katika kipindi maalumu cha Siku 100 za Serikali ya Awamu ya Tano kinachorushwa na kituo cha televisheni cha TBC1 cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
“Katika kipindi cha siku 95, tumeweza kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambazo watumishi wa halmashauri wangezitumia katika safari za ndani zisizo na tija na hazijalenga kumkomboa mwananchi huyu ambaye hana dawa na hana barabara,” alisema Simbachawene.
Akizungumzia uwajibikaji wa watumishi katika halmashauri nchini, Simbachawene alisema ili kuhakikisha halmashauri hizo zinafanya kazi ipasavyo, wameunda kitengo cha ukaguzi ambacho kina kazi ya kudhibiti na kufuatilia utendaji wa kazi za halmashauri.
“Tamisemi tuna deni kubwa, kwani sisi ndio tunaotegemewa na wizara kutafsiri mipango yao ya elimu afya, miundombinu na sekta nyingine. Tamisemi ni wakala wa serikali kwa wananchi,” alisema na kuongeza kuwa watendaji wa halmashauri ambao hawataki kwenda na kasi ya Rais Magufuli, basi wataondolewa katika nafasi zao bila kuonewa haya.
“Tutahakikisha tunawachukulia hatua wezi wote, wabadhirifu na wasio waadilifu, huwezi utupishe. Tutawapima kwa jinsi wanavyoondoa kero kwa wananchi,” alisema na kukiri kuwa katika halmashauri kuna matatizo ya uadilifu jambo linalofanya miradi mingi kushindwa kukamilika na ikikamilika inakuwa chini ya kiwango.
Aidha, amewataka wakurugenzi kuhakikisha wanawafikia wananchi na kumaliza kero za wananchi kinyume chake kazi wataiona chungu.
Kuhusu ukusanyaji wa mapato, Simbachawene alisema asilimia 95 ya halmashauri zote zimeanza kutumia mfumo wa elektroniki katika kukusanya mapato na kuwa zile chache ambazo hazijaanza zimetakiwa kufanya hivyo baada ya kuongezewa muda kidogo

Monday, February 22, 2016

WAENDESHA VYOMBO VYA MOTO BARABARANI WAONYWA KUZINGATIA KUDUMISHA AMANI KWA KUFUATA SHERIA ZA BARABARANI

Dereva bodaboda  wa mtaa wa kwa morombo jijini Arusha

Wamiliki   na   waendesha   vyombo   vya   moto  barabarani   mkoani  Arusha wameombwa   kudumisha    mahusiano    mazuri    na   jeshi la polisi  hasa  kitengo cha  usalama  barabarani

 Kauli    hiyo  imetolewa    mbele    ya  waandishi  wa habari  na kamanda wa usalama    barabarani  mkoani  Arusha Bwana  Malsoni  Mwakyoma   nakusema ajali   zimeendelea  kupungua
.
Kamanda    Mwakyoma    amesema   mahusiano    mazuri   kati  ya  jeshi     la polisi kitengo cha usalama   barabarani  pamoja  na  madereva  ndio  imekuwa    chachu  ya kupunguza  ajali za barabarani  mkoani   Arusha.

Mbali   na  hayo  amesema   sheria  itaendelea  kuchukua mkondo  wake ipasavyo  hasa  kwakukabiliana  na  changamoto    ya ongezeko   la  vyombo  vya  barabarani  pamoja  na ongezeko   la  watumiaji  wa barabara.

VIlevile   amewashukuru   wachungaji  na mashehe  kwa   kuendelea  kuhubiri  amani  na kuwataka   waumini  kuzingatia    alama  na  sheria  za barabarani

Hata hivyo kamanda mwakyoma   ameomba   abiria kutoa taarifa mapema hasa wanapoona    kuna   uvunjifu  wa sheria barabarani    na  kuwataka  wananchi   watii  sheria za usalama  barabarani

Nao  wamiliki  wa  magari  na bodaboda    pamoja   na  madereva  bila  kusahau   wananchi wamemshukuru  kamanda  Mwakyoma     kumhakikishia  kuwepo  uhusiano mwema   katika  uwajibikaji.



  

LA LIGA; UBINGWA REAL MADRID NI NDOTO




Image copyrightAFP
Image captionKocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane

Klabu ya soka ya Real Madrid kwa mara nyingine tena imetoshana nguvu na Malaga kufuatia sare ya 1-1 katika mchezo uliopigwa jana na kupelekea kuwa pointi 9 nyuma ya mahasimu wao Barcelona ambao walishinda dhidi La Palmas bao ya 2-1.
Huku kocha zinedine Zidane akiwa na kikosi kilichokuwa na upungufu wa Karim Benzema na Gareth Bale akimuanzisha Cristiano Ronaldo ambaye ndiye aliyeifungia bao Madrid dakika 33.
Dakika 2 baadaye Madrid wakapata penati ambayo Cristinao Ronaldo akaipoteza baada ya kuokolewa na kipa wa Malaga – Carlos Idriss Kameni.
Dakika ya 66, Raul Albentosa aliisawazishia Malaga kwa assist nzuri ya beki wa kati Welington na kuufanya mchezo usomeke kwa matokeo wa ba 1-1 hadi mwisho wa mchezo.
Hii inakuwa penati ya 7 kwa Ronaldo kukosa msimu huu,ikiwa ni idadi sawa na mpinzani wake Lionel Messi

Thursday, February 18, 2016

RONALDO AWAJIBU WAANDISHI KWA VITENDO

Ronaldo awajibu waandishi kwa vitendo

  • 18 Februari 2016

Image copyright
Image captionChristiano Ronaldo

Christian Ronaldo ni kama amewajibu kwa vitendo wanahabari wale ambao jumanne alikataa kuendelea kuongea nao pale alipoulizwa kuhusu ukame wa magoli ya ugenini. Goli lake la 33 la Musimu limeisaidia Real Madrid kusogelea robo fainali ya Champions Ligi. Kikosi kilichoko chini ya Zinedine Zidane kimeichapa Roma bao mbili kwa moja.
Kabla ya Mechi hiyo Mshambuliaji huyo alikuwa ameondoka kwa hasira katika katika chumba cha mahojiano baada ya kuulizwa juu ya rekodi ya ufungaji magoli katika mechi za ugenini msimu huu.
Ronaldo mwenye miaka 31, mpaka hapo alikuwa amefunga magoli 32 msimu huu lakini hakuwa amefunga nje tangu mwezi Novemba. "Nani mwingine amefunga magoli mengi ugenini kuliko mimi tangu nimekuja Hispania?Ronaldo mfungaji namba moja wa Championzi Ligi aliuliza kwa kukereka" Taja mchezaji mmoja ambaye amefunga kuliko mimi. Hakuna jibu? Sawa. Asante" Akaondoka

Wednesday, February 17, 2016

MAJIPU YAENDELEA KUTUMBULIWA KATIKA MIKOA TOFAUTI TOFAUTI NCHINI

WAZIRI nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mtaa,George Simbachawane amewasimamisha kazi wakurugenzi wa nne  kwa  tuhuma  za  kuwahonga wakaguzi wa fedha  kutoka katika ofisi ya Mkaguzi mkuu wa  Hesabu za  serikali (CAG) ili wapewe hati  safi huku Halmashauri hizi zikiwa na ufisadi .

Wakurugenzi  waliosimamishwa  kazi  ni   Elizabeth Chitundu wa Halmashauri za Misenyi mkaoni Kagera, Ally Kisengi wa Halmashauri ya Nanyumbu mkaoni Mtwara  na  Abdalla Mfaume wa Halmashauri ya Mbogwe mkoani Geita.

Pia,Waziri Simbachawene   amemsimamisha kazi  mkurugenzi Halmashauri ya  Tunduma Mkoani  Mbeya Bi Halima Ajali  ili kupisha uchunguzi kutokana matumizi mabaya ya madaraka ikiwa ni pamoja na kuwatumia watoto wake katika shuguli za halmashauri na kuwalipa posho na kusababisha upotevu wa mapato.

Aidha, Waziri Simbachawane pia ameziagiza mamlaka husika kuwasimisha kazi watendaji wa ofisi ya mkaguzi wa Hesabu za Serikali nchini,CAG  waliohusika kupokea rushwa kutoka kwa wakurugenzi hao ili watoe  hati safi kwenye Halmashauri hizo huku zikiwa na ubadilifu wa fedha za Umma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mchana Jijini Dar es Salaam,Waziri Simbachawene amesema Wakurugenzi hao wamegundulika  baada ya uchunguzi wa kina uliofanywa na wizara yake

Akibainisha makosa ya kila mkurugenzi,Waziri Simbachawene amesema Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misenyi, Bi Chitundu  alimwagiza  mweka hazina wake Majaliwa Bikwato atoe rushwa ya Milioni tatu kwa maafisa wa  ofisi ya CAG kwa lengo la kuficha kasoro walizoziabini katika ukaguzi huo  huku akijua ni kosa kisheria. Watumishi wa  wa ofisi ya CAG  waliopokea pesa hizo ni Stevin Buawa,John Elias pamoja na Kilembi Mkole

Katika Halmashauri ya Nanyumbu, Simbachawene amesema  kuwa  tarehe 26 Juni 2015, mkurugenzi wake bwana Kasengi pamoja na mweka hazina Pasco Malowo na mwasibu Emmanuel Mugesa walimkabidhi fedha Milioni 3 na laki tano  afisa wa ofisi ya  CAG  kwa lengo la kutoa hati safi

Waziri Simbachawene amesema mwezi Novemba mwaka jana , Mkurugenzi wa Halmashauri  ya  Mbogwe mkoani Geita Abdalla Mfaume na mweka hazina wake waliwapatia milioni 16  maafisa wakaguzi wa ofisi ya CAG  ili wafiche ufisadi walioubaini

Amesema katika Halmashauri hiyo pia kumegundulika kuwepo na ufisadi mkubwa ikiwemo malipo ya mishahara hewa pamoja na malipo ya milioni 200 yaliotolewa pasipo kuwa na Stakabadh

UCHAFU ULIYO KITHIRI MAENEO MBALIMBALI KATIKA JIJI LA ARUSHA



uchafu katika katika kata ya sokoni one mtaa wa ololovono 



Wananchi  jijini Arusha  wameulalamikia  uongozi  kuhusu suala zima la usafi hasa uwepo wa takataka katika mitaa yao.
Hayo yamesemwa na wananchi wa mtaa wa ololovono kata ya sokoni one  Bw. Macha Molel na B.Elizabeth Ngowi walipokuwa wakizungumza na Mgonja blog  leo hii na kutoa dukuduku zao
Wamesema   mtaa  wao  una  uchafu  mwingi na ambao husababisha magonjwa ya mlipuko kama vile homa ya matumbo pamoja na kipindupindu.
Pia wananchi hao wameulalamikia uongozi kwa kutoshughulikia suala la usafi ipasavyo  hasa mzabuni ambaye  amepewa    jukumumu  hilo la kupeleka takataka katika eneo husika ambapo mara nyingi huchelewa  wakati huo huo wananchi wanalipia  shilingi   1500 kila mwezi kwa ajili ya usafi.
Naye mwenyekiti  wa mtaa huo Yelome Wambura  amekiri  kuwa  kuwepo  kwa uchafu katika mtaa wake ambapo amesema mojaya sababu  ni wananchi kutojal i suala la usafi na  kusahau kuwa  usafi ni af ya.
Pia  amelalamikia  wananchi kutokuwa na elimu  ya kutosha  kuhusu utunzaji  wa mazingira ambapo baadhi  yao hutupa takataka hasa mifuko ya malboro katika mitaro ya maji  na kupelekea  mitaro kuziba.
Vilevile amelalamikia suala zima la utoaji sabuni na kusema kuwa hutolewa kwa upendeleo ambapo hupelekea mzabuni kufanya kazi  kwa matakwa yake yaani bila kufuata maelekezo husika.  
Mwenyekiti    huyo ameiasa  serikali kutilia mkazo suala la usafi kwani usafi ndio nguzoya afya  bora na kuitaka kusambaza  vizimba kila mtaa  kwaajili  ya  kuweka takataka.


Tuesday, February 16, 2016

ELIMU YA UJASIRIAMALI VYUONI



Wanafunzi  wa  vyuo  vikuu  pamoja  na  vyuo  cha  kati nchini wameshauriwa kujihusisha na  masuala  mbalimbali  ikiwemo uchumi.

Hayo  yamesemwa na mkurungezi  wa  mafunzo  wa  chuo  cha  uandishi  wa habari na  utangazaji Arusha  Bwana Joseph Mayagila  wakati   akitoa semina ya mafunzo ya ujasiriamali katika  ukumbi wa chuo hicho.

Bwana Mayagila amesema kuwa ni vyema kila mwanafunzi  kujitafutia akiba ya kumwezesha pale atakapokwama katika mahitaji yake ya kila siku.

Amesema zipo njia mbalimbali za kujipatia mahitaji kwa kila mwanafunzi ukiachilia mbali ada kwani mwanafunzi anaweza kuanzisha biashara kidogokidogo mpaka pale itakapokuwa.

“Mwanafunzi anatakiwa kuwa mjasiriamali kwani anaweza kuuza vitu vidogovidogo kama pipi, kuwa mwanamuziki, kuuza nguo na maitaji mengine ambayo yanaitajika katika eneo la chuo”.

Aidha amesema ili kuweza kupata mtaji wa kuweza kuanzisha biashara ni vyema kujijengea mazoea ya kuwekeza kiasi kidogokidogo cha hela kila siku ili kuweza kufikia malengo.

Ameongeza kuwa kila mjasiriamali anatakiwa kusoma vitabu mbalimbali vya ujasiriamali ili kuweza kupata mbinu mbalimbali za kuendeleza biashara zao.
Baadhi  ya wanafunzi wa vyuo vya kati wamesema elimu za ujasiriamali zimewapa mbinu mbalimbali za kuweza kukabiliana na changamoto zinazowakabili katika biashara zao.

“Elimu au mafunzo haya yametufikisha mbali kiuchumi kwani tulikuwa tukianzisha biashara zinakufa lakini saizi hatupati shida hata kidogo kwani tumepata ufumbuzi zaidi”

Hata hivyo elimu hiyo imewawezesha baadhi ya wanafunzi kuwa na maisha mazuri kwani wamejiingiza katika masuala ya ujasiriamali na kuweza kujipatia mahitaji yao ya kila siku.