Taasisi na makampuni
binafsi nchini wameaswa kuboresha na
kuimarisha ulinzi kwa lengo la
kujihami na maadui wanaojitokeza.
Hayo yamesemwa na Kamanda
wa polisi wa polisi jiji la Arusha Bw. Liberatus Sabas wakati alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Kamanda wa polisi mkoani Arusha Bw. Liberatus Sabas
Hata hivyo amewasisitiza wamiliki wa taasisi na makampuni
binafsi kuweka ulinzi wa kutosha na
wenye uhakika na kuchukua na kuchukua walinzi kutoka kwenye makampuni ya ulinzi
yenye vitendea kazi vya kisasa.
Vilevile amewataka wananchi kutoa taarifa mapema hasa zile
wanazozitilia mashaka kwa ajili ya
kulinda na kuboresha amani.
Pia amewaasa
wananchi kujichukulia sheria mkononi kwani zinajaribu kupata
mtandao mzma wa kuharifu na kuwataka watoe taarifa katika vyombo vya habari
nchini.
Nao baadhi ya wamiliki wa hoteli jijini Arusha Bw. Saimoni
Mrema na Bw. Vanley Gopal wamelishukuru jeshi la polisi kwa kuimarisha ulinzi katika viunga
hapa jijini Arusha na
kuwahakikishia utakuwa wakutosha.
No comments:
Post a Comment