Dereva bodaboda wa mtaa wa kwa morombo jijini Arusha
Wamiliki na
waendesha vyombo vya moto barabarani mkoani
Arusha wameombwa kudumisha
mahusiano mazuri na jeshi
la polisi hasa kitengo cha
usalama barabarani
Kauli hiyo
imetolewa mbele ya waandishi wa habari
na kamanda wa usalama
barabarani mkoani Arusha Bwana Malsoni
Mwakyoma nakusema ajali zimeendelea
kupungua
.
Kamanda
Mwakyoma amesema mahusiano
mazuri kati ya
jeshi la polisi kitengo cha
usalama barabarani pamoja
na madereva ndio
imekuwa chachu ya kupunguza
ajali za barabarani mkoani Arusha.
Mbali na hayo
amesema sheria itaendelea
kuchukua mkondo wake ipasavyo hasa kwakukabiliana na
changamoto ya ongezeko la
vyombo vya barabarani
pamoja na ongezeko la
watumiaji wa barabara.
VIlevile
amewashukuru wachungaji na mashehe
kwa kuendelea kuhubiri
amani na kuwataka waumini
kuzingatia alama na
sheria za barabarani
Hata hivyo kamanda mwakyoma
ameomba abiria kutoa taarifa
mapema hasa wanapoona kuna uvunjifu
wa sheria barabarani na kuwataka
wananchi watii sheria za usalama barabarani
Nao wamiliki wa
magari na bodaboda pamoja
na madereva bila
kusahau wananchi
wamemshukuru kamanda Mwakyoma
kumhakikishia kuwepo
uhusiano mwema katika uwajibikaji.
No comments:
Post a Comment