Thursday, February 25, 2016

Wanafunzi waliochochea wenzao wajisalimisha India




Image caption

Wanafunzi wawili wa kihindi waliodaiwa kuwachochea wanafunzi wa chuo kikuu cha Jawaharlal Nehru kuandamana huko Delhi wamejisalimisha kwa polisi wenyewe.
Umar Khalid na Anirban Bhattacharya ni miongoni mwa wale waliokuwa wakitafutwa na polisi.
Kukamatwa kwa kiongozi wa muungano wa wanafunzi wa chuo hicho Kanhaiya Kumar, mapema mwezi huu ndiko kulikosababisha ghasia katika sehemu nyingi nchini India.
Baada ya Bwana Kumar kukamatwa, wanafunzi wengine ambao wametajwa kuhusiana na maandamano hayo walitoweka lakini wakajitokeza katika chuo kikuuu cha JNU siku ya Jumapili usiku.
Polisi hawakuingia katika chuo hicho lakini jumanne usiku Umar Khalid na Anirban Bhattacharya waliondoka katika chuo hicho kwa hiari na kujisalimisha kwa polisi.
Polisi hawaruhusiwi kuingia vyuoni bila idhini ya viongozi wa chuo,ripoti zimesema.
Polisi wamewata wanafunzi waliosalia - Ashutosh Kumar,Anant Prakash Narayan, Riyazul Haq na Rama Naga -kujisalimisha

No comments:

Post a Comment