Wazazi na walezi nchini wameaswa kuheshimu haki za watoto na kujua kwamba suala la kuhudumia watoto sio hiari ya mtu bali ni lazima kwa mujibu wa sheria.
Hayo yamesemwa na Afisa wa ustawi wa jamii wa jiji la Arusha Mr Shija Numbu wakati akiongea na mgonja blog ofisini kwake.
Amesem baadhi ya jamii za kiafrika humnyima mtoto haki yake kwani mtoto hutolewa mahari akiwa tumboni mwa mama yake hali ambayo humpelekea baadae kuolewa akiwa na umri mdogo lakini pia kuolewa na mtu ambaye pengine hajampenda.
''Kesi za ndoa za utotoni tunazipokea hapa kwa sababu ya mila za kimaasai kwamba mtu anatolewa mahari akiwa tumboni akizaliwa wa kike akifikisha miaka saba[7 ] akachukua mke wake baadae ustawi wa jamii wakajua na kuweza kufuatilia suala hili''
Kwa kuzingatia sheria ya haki ya mtoto.ya mwaka 2009 amesema mtoto ana haki ya kukaa na wazazi wake mpaka pale atakapotimiza umri wa miaka kumi na nane [18] na kuendelea .
Ameongeza kuwa watoto wote wana haki sawa kwani kila mtoto ana haki ya kupata kila aina ya hitaji atakalohitaji.
Mr shija amesema watoto wote wana haki sawa katika katika suala zima la ndoa za utotoni kwani vipo vipengele vinavyomlinda mtoto wa kike lakini pia vipo vya kumlinda mtoto wa kike.
''Sheria ya mwaka 2008 mtoto chini ya umri wa miaka 18hairuhisiwi kuolewa kwani ni sawa na ubakaji, na kwa upande wa mtoto wa kiume sheria inasema hajabaka bali kamnyonya mtoto kingono.
No comments:
Post a Comment