Wednesday, February 24, 2016

BESIGYE; NILIKAMATWA MARA NNE


Image copyrightAP
Image captionKiongozi wa Upinzani wa Chama cha FDC, Kizza Besigye

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kiiza Besigye ameiambia BBC Kuwa ametiwa mbaroni na polisi mara nne kwa muda wa siku sita kufuatia uchaguzi uliofanyika nchini humo wiki iliyopita. Matokeo ya uchaguzi huo yalimpa ushindi Rais Yoweri Museven kutawala nchi hiyo kwa muhula wa tano.
Bwana Besigye ambaye yupo kizuizini nyumbani kwake ameeleza jinsi alivyokamatwa na polisi.
"nilikamatwa na polisi nikiwa nyumbani mwendo wa saa kumi na moja alfajiri, na kupelekwa kwa mwendo kasi mjini ambao ulikuwa ni mwendo wa kutisha ili kuwakwepa waandishi wa habari waliokuwepo katika eneo walinikamata, na hii ilkawa ni mara ya nne kukamatwa na polisi kwa muda wa siku sita."
Besigye amesema amesikitishwa sana kwamba jamii ya kimataifa haijaingilia kati suala hilo kwa niaba yake. Ameonya kwamba kama wanadhani Rais Museveni ameleta amani na utulivu nchini Uganda wajue wanafanya makosa.
"Amani na utulivu ni upande mmoja wa sarafu. Upande wa pili wa sarafu ni haki. Hauwezi kuwa na amani na utulivu bila haki. Na hii ndio hali halisi katika mazingira yetu ni kwamba kwa kifupi hakuna haki "alieleza

No comments:

Post a Comment