Wanafunzi wa vyuo vikuu
pamoja na vyuo
cha kati nchini wameshauriwa kujihusisha na masuala mbalimbali ikiwemo uchumi.
Hayo yamesemwa na mkurungezi wa mafunzo
wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha Bwana Joseph Mayagila wakati akitoa semina ya mafunzo ya ujasiriamali
katika ukumbi wa chuo hicho.
Bwana Mayagila
amesema kuwa ni vyema kila mwanafunzi
kujitafutia akiba ya kumwezesha pale atakapokwama katika mahitaji yake
ya kila siku.
Amesema zipo
njia mbalimbali za kujipatia mahitaji kwa kila mwanafunzi ukiachilia mbali ada
kwani mwanafunzi anaweza kuanzisha biashara kidogokidogo mpaka pale
itakapokuwa.
“Mwanafunzi
anatakiwa kuwa mjasiriamali kwani anaweza kuuza vitu vidogovidogo kama pipi,
kuwa mwanamuziki, kuuza nguo na maitaji mengine ambayo yanaitajika katika eneo
la chuo”.
Aidha
amesema ili kuweza kupata mtaji wa kuweza kuanzisha biashara ni vyema
kujijengea mazoea ya kuwekeza kiasi kidogokidogo cha hela kila siku ili kuweza
kufikia malengo.
Ameongeza
kuwa kila mjasiriamali anatakiwa kusoma vitabu mbalimbali vya ujasiriamali ili
kuweza kupata mbinu mbalimbali za kuendeleza biashara zao.
Baadhi ya wanafunzi wa vyuo vya kati wamesema elimu
za ujasiriamali zimewapa mbinu mbalimbali za kuweza kukabiliana na changamoto
zinazowakabili katika biashara zao.
“Elimu au
mafunzo haya yametufikisha mbali kiuchumi kwani tulikuwa tukianzisha biashara
zinakufa lakini saizi hatupati shida hata kidogo kwani tumepata ufumbuzi zaidi”
Hata hivyo
elimu hiyo imewawezesha baadhi ya wanafunzi kuwa na maisha mazuri kwani
wamejiingiza katika masuala ya ujasiriamali na kuweza kujipatia mahitaji yao ya
kila siku.
No comments:
Post a Comment