uchafu katika katika kata ya sokoni one mtaa wa ololovono
Wananchi jijini
Arusha wameulalamikia uongozi
kuhusu suala zima la usafi hasa uwepo wa takataka katika mitaa yao.
Hayo yamesemwa na wananchi wa mtaa wa ololovono kata ya
sokoni one Bw. Macha Molel na
B.Elizabeth Ngowi walipokuwa wakizungumza na Mgonja blog leo hii na kutoa
dukuduku zao
Wamesema mtaa wao una
uchafu
mwingi na ambao husababisha magonjwa ya mlipuko kama vile homa ya
matumbo pamoja na kipindupindu.
Pia wananchi hao wameulalamikia uongozi kwa kutoshughulikia
suala la usafi ipasavyo hasa mzabuni
ambaye amepewa jukumumu
hilo la kupeleka takataka katika eneo husika ambapo mara nyingi
huchelewa wakati huo huo wananchi
wanalipia shilingi 1500 kila mwezi kwa ajili ya usafi.
Naye mwenyekiti wa
mtaa huo Yelome Wambura amekiri kuwa
kuwepo kwa uchafu katika mtaa
wake ambapo amesema mojaya sababu ni
wananchi kutojal i suala la usafi na
kusahau kuwa usafi ni af ya.
Pia amelalamikia wananchi kutokuwa na elimu ya kutosha
kuhusu utunzaji wa mazingira
ambapo baadhi yao hutupa takataka hasa
mifuko ya malboro katika mitaro ya maji
na kupelekea mitaro kuziba.
Vilevile amelalamikia suala zima la utoaji sabuni na kusema
kuwa hutolewa kwa upendeleo ambapo hupelekea mzabuni kufanya kazi kwa matakwa yake yaani bila kufuata maelekezo
husika.
Mwenyekiti huyo
ameiasa serikali kutilia mkazo suala la
usafi kwani usafi ndio nguzoya afya bora
na kuitaka kusambaza vizimba kila
mtaa kwaajili ya
kuweka takataka.
No comments:
Post a Comment